*Atoa msamaha kwa wafungwa 4400, awapongeza awamu zote 
zilizopita
*Asisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana kujenga uchumi wa nchi 
yetu

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli amewatakia Watanzania wote nchini kutafakari tulikotoka, tulipo na tunakokwenda huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kufanya kazi ili kujenga uchumi imara hasa kwa kuzingatia kwa sasa tupo kwenye vita ya kiuchumi ambayo lazima wote tushirikiane kuishinda.

Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati anatoa salamu za kuwatakia kila laheri Watanzania katika kuelekea kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 2018 ambapo itakuwa Jumapili ya wiki hii na kufafanua siku hiyo itakuwa ni ya mapumziko, ambayo itumike kutafakari tulikotoka na tunakokwenda.

"Kila laheri Watanzania katika kusherehekea miaka 57 ya Uhuru wa Tanganyika.Kama ambavyo mnafahamu tayari fedha Sh.bilioni moja 
zilitengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo lakini nimeshatoa maelekezo fedha hizo zitumike kujenga Hospitali Dodoma ambayo itaitwa Hospitali ya Uhuru,"amesema Rais Dk.Magufuli na kufafanua kwa kuwa Serikali inahamia Dodoma kuna umuhimu wa kujengwa kwa hospitali nyingine ili ziwepo mbili,"amesema.

Amesema kuwa tayari sehemu ya watumishi wa Serikali wapo Dodoma na amebaki yeye tu ambaye naye anajiandaa kuondoka siku za hivi karibuni na hivyo ndio maana ni muhimu kujengwa kwa hospitali ya pili ili isaidiane na Hospitali ya Mkapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...