Serikali imewaagiza viongozi wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kata ya Parakuyo kuhakikisha wanawaondoa wavamizi waliovamia Ranchi ya Narco Mkata. Agizo ilo limetolewa na Naibu waziri wa mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati alipokuwa anafanya ziara wilaya Kilosa kwa lengo la kusikiliza kero za wafugaji. "Msimuonee mtu ambae analima nje Ranchi NARCO na hakikisheni mnawapokonya vitalu waliopewa wakashindwa kuviendeleza ili wapewe wafungaji wengine alisema Ulega"

Mhe Ulega aliwaeleza wafugaji maagizo yake kwa viongozi wa wilaya juu ya kuwaondoa wavamizi katika Ranchi ya NARCO Mkata na wote wanaolima katika maeneo hayo na wakodishiwe wafugaji kwa ajili ya kunenepesha Mifugo yao katika vitalu vitakavyokuwa vimeandaliwa. Alisema Wilaya inakuja na majina ya wafugaji na idadi ya mifugo yao wanaohitaji vitalu hivyo. 

"Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na Rais wetu anawapenda sana wafugaji na watu wote anatupenda na alishatupa maagizo kama wizara kuwaondoa watu waliohodhi maeneo ya Ranchi na kuwapa wafugaji wetu"
Wakati Mhe. Ulega akijibu hoja ya wafugaji kukosa elimu ya ufugaji wa kisasa wenye tija ikiambatana na elimu ya uzalishaji wa malisho aliwaagiza wataalam wa mifugo kutoka Wakala wa Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Mifugo (LITA) alioongozana nao katika ziara hiyo kupeleka wanafunzi kujifunza kwa vitendo katika kata ya Parakuyo na maeneo mengine ya wafugaji ili waweze kusambaza elimu hizo kwa wafugaji kuliko wanafunzi hao kufanya  mafunzo hayo maeneo ya mijini.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafungaji  katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Parakuyo wilaya Kolosa mkoa wa Morogoro ambapo amewahakikishi kuwa Serikali  itaendelea kuboresha miundombinu,majosho mabirika ya maji.

Baadhi ya wafungaji wa wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro  wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.
 Meneja wa Rachi ya Mkata wilaya ya Kilosa, Sadalah Athuman(kulia) akitoa taarifa  fupi ya mikakati waliyoiweka kuwasaidia wafungaji wa  wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...