THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia

Na Mwandishi Wetu
Serikali imesisitiza uwepo wa usawa wa kijinsia katika sekta mbalimbali ili kuendelea kuunga jitihada za kuwezesha usawa huo ambao uliasisiwa katika Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake uliofanyika Beijing nchini China mwaka 1995 huku ikisisitiza ni muhimu kuundwa kwa madawati ya jinsia katika idara za serikali.

Hayo yamesemwa na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizindua   Mtandao  wa  Wanawake  na  Utambulisho  wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza leo  jijini Dar es Salaam .

Amesema Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha usawa wa kijnsia unafikiwa katika sekta na nyanja mbalimbali kwa kuchukua hatua ikiwemo kuandaliwa kwa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 pamoja na Mkakati wa Utekelezaji wake kwa lengo la kuweka mazingira muafaka na kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia yanzingatiwa na wadau ikiwemo Wizara, Idara na Wakala  za Serikali, Mamlaka  za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili  kushoto), na Viongozi  Waandamizi  wa  Jeshi  la Magereza  wakikata utepe  kuashiria  Uzinduzi  wa  Mtandao  wa  Wanawake  na  Utambulisho  wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza. Uzinduzi huo umefanyika leo katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati) akimkabidhi tuzo Mwakilishi wa Benki ya NMB,ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo ya kifedha  katika uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati), akimkabidhi tuzo mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Wanawake(TAWLA), ikiwa  ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo katika uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia bidhaa inayotengenezwa na Jeshi la Magereza  wakati alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia bidhaa zinazotengenezwa  na Jeshi la Magereza  wakati alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzunduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA