SERIKALI imepongeza mradi wa XPRIZE kwa kuonesha njia nyingine ya kuwapatia elimu ya kusoma, kuandika na kuhesabu watoto wengi walio nje ya mfumo rasmi wa elimu. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wakati alipotembelea wilaya ya Mkinga, ikiwa ni mojawapo ya wilaya sita (6) za Mkoa wa Tanga, zinazonufaika na mradi huo. 
Akizungumza katika mahojiano, Katibu Mkuu huyo alisema kwamba kinachowaondoa watoto wengi katika masomo si lazima iwe mimba kwani wapo watoto wengi hasa wakiume ambao wanakimbia majumbani na kukosa haki yao ya msingi ya elimu. “Huu mradi umetuonesha njia nyingine kabisa ya kukabiliana na tatizo hili. “ anasema Dk Akwilapo ambaye amesema ni sera ya serikali ya kuhakikisha kwamba watoto wote hata wale ambao hawakuingia katika mfumo rasmi wanaingiza katika mfumo wa elimu kwa kupitia taratibu mbalimbali. Miongoni mwa taratibu hizo ni utaratibu wa MEMKWA kwa elimu ya msingi na MESPA kwa sekondari. Alisema mradi huo wa MEMKWA umeonesha matokeo mazuri kwa sasa kwani tayari watoto 800 wamefikishwa katika shule wakafanyiwa mitihani na kuingizwa kuendelea na madarasa ya pili.
Mradi wa XPRIZE ambao utamalizika mwaka kesho ukitumia vishkwambi katika mafunzo kwa watoto waliokosa elimu ya msingi kufikia miaka 9, ni mradi wa dunia ambapo teknolojia inajaribiwa kusaidia wale waliokosa nafasi ya kuingia shule. Akizungumzia hatima ya mradi huo, Mwakilishi wa Global Learning Xprize, Elianne Philibert  alisema kwamba mafanikio yake yatawezeshwa kutengenezwa kwa moduli za kufundishia watoto walio nje ya mfumo rasmi wanaotumia lugha ya Kiswahili.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akibadilishana mawazo na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham mara baada ya kuwasili katika ofisi za mkoa wa Tanga mwishoni mwa juma wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE mkoani humo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos, Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham pamoja na Mwakilishi wa Global Learning Xprize, Elianne Philibert  wakipokea taarifa fupi kwenye ofisi za Kaimu Katibu Tawala wa  mkoa wa Tanga Bi Monica Kinanan kabla ya kuelekea kukagua mradi wa XPRIZE uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (kulia), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos(kushoto) wakipata maelezo ya kifaa maalum kinachotumia umeme wa jua kuchajia Vishkwambia kutoka kwa Mtaalamu wa Tehama wa mradi wa XPRIZE Tanga, Bw. Xavery Njovu wakati wa ziara ya kukagua mradi huo uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akiangalia jinsi mmoja wa watoto wa kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga walio nje ya mfumo rasmi wa elimu anavyojifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia Vishkwambi hiyvo wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham wakitazama jinsi watoto wa kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga walio nje ya mfumo rasmi wa elimu wanavyojifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia Vishkwambi hiyvo wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE mkoani humo mwishoni mwa juma.oa wa Tanga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...