Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi ametoa vyeti vya mafunzo ya muda mfupi kwa mafundi simu za mkononi waliohitimu mafunzo hayo kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe
“Nawapongeza mafundi simu wa kike watatu kwa kuwa suala la ufundi linachukuliwa kuwa ni la wanaume, naamini ninyi watatu mtakuwa chachu kwa wanawake wengine kujiunga na mafunzo haya,” amesema Dkt. Yonazi wakati akitoa vyeti kwa mafundi simu za mkononi 68 waliohitimu mafunzo hayo ambapo kati yao watatu ni wanawake waliohudhuria mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Julai mwaka huu. Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa mafundi simu za mkononi kwa kuwa yatawawezesha kulinda usalama wa taarifa, yataleta tija na kuweza kuingiza fedha za kigeni kupitia Sekta ya Mawasiliano.
Amefafanua kuwa mafunzo hayo yako sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo Serikali imejipanga kutekeleza Ilani hiyo kupitia kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya ujenzi wa viwanda ambapo tayari Kampuni ya IPP Touchmate Tanzania Ltd itajenga kiwanda cha simu za mkononi nchini na wako tayari kuwapa ajira wahitimu hao kwa kuwa ni mafundi simu wa kwanza nchini kupata mafunzo hayo rasmi
Naibu
Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kulia) akikabidhi cheti kwa
Mwanahamis Abdul Salim aliyehitimu mafunzo ya kutengeneza simu za
mkononi kwenye Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Anayeshuhudia
wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo, Mulembwa Munaku
Naibu
Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na mafundi simu za mkononi wa kike watatu (waliosimama) kati ya
68 waliohitimu mafunzo DIT, Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi
wa TEHAMA, Wizara hiyo Mulembwa Munaku na wa kwanza kushoto ni Kaimu
Mkuu wa Taasisi ya DIT, Prof. Patrick Nsimama
Naibu
Katibu Mkuu Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja
na meza kuu na wadau waliohudhuria hafla ya utoaji vyeti na leseni kwa
mafundi simu za mkononi wa kwanza waliohitimu mafunzo yao, Taasisi ya
DIT, Dar es Salaam. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo
Mulembwa Munaku na wa pili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Taasisi ya DIT,
Prof. Patrick Nsimama
Naibu
Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na mafundi simu za mkononi waliohitimu mafunzo hayo kwenye
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam na baadhi ya wadau wa Sekta hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...