.
Na Anitha Jonas,Dodoma

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki wanaoshiriki Mashindano ya vyuo vikuu Kanda ya Afrika Mashariki kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu katika Michezo.

Mheshimiwa Shonza ametoa tamko hilo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mashindano hayo yatakayo dumu kwa wiki mbili nchini ambapo mashindano hayo yamehusisha vyuo takribani ishirini huku lengo la mashindano likiwa ni kuimarisha Umoja na Ushirikiano kwa wanachama wa umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

‘’Ninaimani na waamuzi watakaosimamia michezo yote katika mashindano haya kuwa watatenda haki na pale mtakapoona mwamuzi hakutenda haki basi kateni rufaa badala ya kuleta migogoro katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,’’alisema Mhe.Shonza.Kwa upande wa Mlezi wa Umoja wa Shirikisho la Michezo kwa Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Elifas Bisanda aliupongeza uongozi Chuo Kikuu cha Dodoma kwa maandalizi mazuri waliyofanya ili kufanikisha mashindano hayo ya Kimataifa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kanda Afrika Mashariki.

Pamoja na hayo nae Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Prof.Ahmed Ame aliwataka wanamichezo hao pamoja na kuja kushiriki mashindano hayo mara badaa ya mashindano wasisite kutembelea vivutio mbalimbali vilivyoko nchini hapa ikiwemo kutembelea vivutio kama mbuga za wanyama pamoja na Michoro ya Kondoa Irangi.
 
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akiwataka wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki waliyoshiriki Mashindano ya Michezo ya Umoja huo kuimarisha Umoja na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki alipokuwa akifungua Mashindano Kumi na Moja ya vyuo vya nchi wanachama leo jijini Dodoma(kushoto ) Rais wa Shirikisho hilo la Michezo kwa Vyuo Vikuu Vya Afrika Mashariki Cyriaco Kabagambe.
PIX 2
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (aliyevaa tisheti ya kijivu na koti nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na wataribu wa mashindano hayo leo jijini Dodoma mara baada ya ufunguzi wa mashindano ya Kumi na Moja ya Michezo kwa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki,aliyevaa track suit nyeusi  ni Naibu Waziri wa Elimu ya Juu na Tafiti za Kisayansi Burundi Mhe.Theophile Ndarufatiye.
PIX 3
Wanamichezo ambao ni wanafunzi  kutoka  Vyuo Vikuu nchini Burundi wakipita kutoa heshima kwa mgeni rasmi Mheshimiwa Naibu Waziri  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati ufunguzi wa mashindano ya Michezo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
PIX 4
Wanamichezo ambao ni wanafunzi  kutoka  Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya wakipita kutoa heshima kwa mgeni rasmi Mheshimiwa Naibu Waziri  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza hayupo pichani wakati ufunguzi wa mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...