Na Joseph Zablon

Jumuia ya Wazazi (CCM), imeanza kutekeleza mpango wa kutoa elimu ya ufugaji nyuki kibiashara kwa wanafunzi wa shule zote zinazomilikiwa na jumuia hiyo na kwa wananchi wa wilaya zote nchini kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi na pia kutoa ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu masomo yao ya sekondari

Akizungumza na waandishi wa habari kufuatia ziara ya hivi karibuni ya kukagua utekelezaji wa mpango huo, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dk Edmund Mndolwa alisema ufugaji nyuki licha ya kuwezesha upatikanaji wa asali lakini pia kuna mazao mengi yanayotokana na wadudu hao.

“Tutalenga kwanza kwenye asali ingawa kuna mazao mengi na yenye thamani kubwa kuliko asali” alisema na kuongeza kuwa ameziagiza shule zote 55 za sekondari za wazazi nchi nzima kuhakikisha hadi Aprili 2019 mazao ya kwanza au kabla ya hapo” alisema mwenyekiti huyo.

Alisema anawapongeza viongozi na watendaji wa shule hizo kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwani utakuwa na mchango mkubwa katika kuitoa ajira kla vijana,jamii, pato la ndani la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni, huanzishwaji wa viwanda vidogo na kupunguza umaskini kwa jamii.

Alisema mpango huo ambao ulibuniwa na yeye mwenyewe, ukakubaliwa na kamati ndogo ya baraza, kisha ukapitishwa na Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi Taifa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kuziendesha shule hizo na kuziimarisha kiuchumi tofauti na ilivyokuwa awali.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi (CCM) Taifa, Dk Edmund Mndolwa (kulia), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuia hiyo jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kuanza kutekeleza kwa mradi wa mafunzo ya ufugaji nyuki mashuleni kwa shule zinazomilikiwa na jumuia hiyo. Picha na Joseph Zablon.

https://michuzi-matukio.blogspot.com/2018/12/shule-za-jumuia-ya-wazazi-ccm.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...