MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha shughuli mbali mbali za jamii, kwa kutoa misaada yenye tija.

Hilo limekuwa bayana leo tarehe 12 Disemba, 2018 kwenye Kijiji cha Makumbosho Jijini Dar es Salaam, ambapo TAA imetoa msaada wa fulana 100 kwa ajili ya kufanikisha Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba, 2018 katika Uwanja wa Mazaina Chato.

Akizungumza katika Mkutano wa waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Bw. Abdi Mkwizu amesema Mamlaka ina wajibu mkubwa wa kuunga mkono shughuli za kijamii, kwa kutoa misaada ya mbalimbali.

“Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ina wajibu wa Kusimamia, kuendesha, kuboresha na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania lakini pia mbali na kutoa huduma hizo tuna wajibu wa kushiriki katika shughuli za kijamii, kwa wadau ambao wanatufanya sisi tuwepo,” amesema Bw. Mkwizu.

Pia Bw. Mkwizu amebainisha kwamba TAA inahudumia Viwanja 58 vilivyopo Tanzania Bara chini ya serikali, hivyo ni wajibu wao kushiriki katika shughuli za kusaidia jamii sehemu yeyote ile kulingana na uhitaji na bajeti iliyopo.
Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajia kufanyika Disemba 22, 2018. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Abdi Mkwizu (kulia) na Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi G;unze (kushoto). Mkutano huo wa waandishi wa habari umefanyika leo katika Kijiji cha Makumbusho. 
Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze (kushoto), Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia) kwa pamoja wakionesha tangazo la tamasha la Utamaduni la Chato lenye kauli mbiu ya “Maendeleo ya Viwanda yasiache Utamaduni nyuma”. Tukio hilo limefanyika leo kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari katika Kijiji cha Makumbusho. 
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia), akikabidhi moja ya fulana 100 zilizotolewa na TAA kwa muandaaji wa Tamasha la Utamaduni la Chato, Bw. Amon Mkoga (kushoto), Katikati anayeshughudia ni Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze. Tamasha hilo litafanyika Disemba 22, 2018. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...