Taasisi ya Dr Reginald MENGI ya kusaidia watu Wenye ulemavu imeamua kutoa tuzo kwa Watu Wenye ulemavu ili kuihamasisha jamii kutambua kuwa  watu hao wana uwezo wa kufanya makubwa.
Akitangaza utoaji wa tuzo hizo za " I can", jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Dr Reginald MENGI Persons with Disabilities, Bi. Shimimana Ntuyabaliwe amesema Tuzo za mafanikio katika maeneo saba tofauti zitatolewa kwa washiriki watakaoshinda baada ya kupitia mchakato wà uteuzi.
Amesema tuzo hizo zimewalenga watu wenye ulemavu waliofanikiwa kwenye nyanja za elimu, siasa, uongozi, ujasiriamali, Sanaa na burudani, michezo, na ujuzi wa kipekee na ametaja sifa za watu wanaostahili kuwania tuzo hizo.
Amesema washindi watatangazwa na kukabidhiwa tuzo hizo, na fedha taslimu tarehe 2 February mwakani wakati wa tafrija ya kila mwaka  ya chakula cha mchana kwa watu wenye ulemavu inayoandaliwa na Dr Reginald Mengi.
Amewataka watu wenye sifa watume mapendekezo yao kwenye Taasisi hiyo kwa njia za barua pepe (info@drmengifoundation.org) , whatsapp +255 692 141 979 na vituo vya ITV/Radio one, ambapo mwisho wa kupokea  mapendekezo hayo ni  January 18, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Dr Reginald MENGI Persons with Disabilities Foundation Bi. Shimimana Ntuyabaliwe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utoaji tuzo za I Can kwa Watu wenye Ulemavu waliofanikiwa kwenye nyanja za elimu, siasa, uongozi, ujasiriamali, Sanaa na burudani, michezo, na ujuzi wa kipekee katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Makao Makuu wa IPP jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mifumo ya Habari wa Taasisi ya Dr Reginald MENGI Persons with Disabilities, Bw. Francis Bazil na kulia ni Meneja wa Utawala na Fedha wa Taasisi ya Dr Reginald MENGI Persons with Disabilities, Bw. Peter Sarungi,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...