Na Karama  Kenyunko, Blogu ya Jamii

KAIMU Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maendeleo  ya Makazi Wilson Luge (39) ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kuwa fedha alizoenda kuhakiki katika ofisi  ya Waziri  wa  Ardhi   zinazodaiwa  kutolewa kama rushwa kwa Waziri William Lukuvi zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko wa kaki.

Luge ameyasema hayo leo  Desemba  11, 2018  wakati anajibu swali la  Wakili  wa utetezi Imani Madega dhidi ya kesi ya tuhuma za rushwa  ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone,Mohamed Kiluwa alipokuwa akitoa ushahidi  wake mbele ya Hakimu Mkazi Samwel Obasi.

Amedai mahakamani hapo kuwa Julia  16 mwaka huu akiwa kazini kati ya saa saba mchana hadi saa 10 jioni, walikuwa wanaangalia mfumo wa kielekroniki wanaoutumia kama unafanya kazi vizuri, Esquires na Kamishna Mkuu wa Ardhi Mary Makondo na kuwaelekeza waende ofisi ya Waziri Lukuvi.

Pia amedai walipoingia walikuta watu mbalimbali huku mezani kukiwa na mfuko wa kaki uliokuwa umefungwa ambao hakujua ndani  yake kulikuwa na nini na kwamba mfuko huo ulifunguliwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru na kutoa fedha ambazo ni mabunda manne ya Dola za Marekani 40,000 ambapo waliwataka  yeye na Hellen Philipo walihakiki fedha hizo.

Mapema akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Takukuru Maghela Ndimbo, shahidi huyo wa sita amedai Julai 16, mwaka huu alikuwa ofisini kwake Kanda ya Dar es Salaam ambayo zamani ilikuwa Makao Makuu ya Wizara hiyo.Alidai kati ya saa saba hadi saa 10 jioni, walikuwa wanaangalia mfumo wa kielekroniki wanaoutumia kama unafanya kazi vizuri ambapo Kamishna Mkuu wa Ardhi, Mary Makondo aliwaita akiwaelekeza waende ofisi ya Waziri Lukuvi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...