Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
TANZANIA imetajwa kuwa kati ya nchi tano ndani ya jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC ambazo zinatoa kipaumbele kwa masuala yanayohusu vijana.

Hayo yameelezwa katika mkutano wa vijana toka nchi za SADC uliofanyika mjini Windhoek, Namibia kati ya tarehe 13 na 15 Disemba 2018 ambapo mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Michezo, Vijana na Huduma za Umma wa Namibia, Mheshimiwa Erustus Uutoni ambaye alieleza nafasi zilizopo kwa  vijana katika ukanda huo.

Sambamba na hilo Uutoni alieleza namna viongozi akiwemo Mwalimu Julius Nyerere walivyotumia vizuri ujana wao kuleta uhuru kwenye nchi za kusini mwa Afrika, na kutoa Wito kwa Vijana wa nchi 16 za SADC kutumia vema ujana kwa maendeleo ya uchumi, siasa na jamii zao.

 Uutoni alieleza kuwa wakuu wote wa chi za SADC wapo tayari kusaidia vijana kufikia ndoto zao wakiwa katika nafasi nzuri kuliko wageni wanaoingia na kupora fursa za vijana na
Aliitaja Tanzania kama msambazaji mkuu wa madawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa nchi zote za SADC na kueleza kuwa Vijana wana nafasi kubwa sana katika maendeleo ya viwanda hasa vya vifaa tiba.

Kwa upande wake Mratibu wa masuala ya jamii na maendeleo ya watu SADC Bi. Duduzile Simelane alieleza kuwa Tanzania imekuwa na utaratibu mzuri wa kufungua fursa za kiuongozi kwa vijana, Lakini pia wizara inayohusiana na masuala ya vijana imewekwa chini ya ofisi ya waziri mkuu na ikiwa na naibu waziri ambaye ni kijana( Hapa akimaanisha Naibu Waziri Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Anthony Mavunde).
Wawakilishi kutoka Tanzania, wakiwa kwenye mkutano wa SADC 2018 uliofanyika Windhoek Namibia, kutoka kushoto ni Charangwa Makwira akifuatiwa na Francis Daudi, Aziza Ngalupia na wa mwisho kulia ni Ernest Seko. 

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...