Na Bakari Kimwanga -DAR ES SALAAM 

TAASISI ya Tony Elumelu (TEF), imetangaza kufungua mzunguko wa tano wa programu ya Wajasiriamali Afrika kuanzia Januari 1, 2019 

Maombi hayo yatatumwa na kushughulikiwa kwenye kwenye jukwaa kubwa la mitandao kwa wajasiriamali wa Afrika, TEFConnect - www.tefconnect.com

Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Tony Elumelu yenye makao makuu yake Lagos, nchini Nigeria ilieleza kwamba kuanzia Januari 1, 2019, saa 12 asubuhi, Tony Elumelu itaanza kupokea maombi ya mzunguko wa tano wa Programu ya Wajasiriamali. Ambapo waombaji 1,000 waliochaguliwa wataunganishwa msimamizi wa sasa wapatao 4,470 katika program hiyo. 

Tangu mwaka 2015, Mpango wa Biashara wa TEF – imekuwa ni kichocheo kiliasisiwa kwa misingi ya Afrika ambapo aina hiyo, imewawezesha wajasiriamali 4,470 wa Afrika, ambao kila mmoja amenufaika kwa kupatiwa Dola 5,000 kila mmoja. Hatua hiyo huenda sambamba na mjasiriamali kuhudhuria mafunzo ya biashara yanayoendeshwa kwa wiki 12, ambao hupata ushauri na uzoefu na kujifunza zaidi mazingira ta Biashara ya Afrika. 

Wanufaika wa Programu wamefanikiwa kuhojiwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Forbes (Afrika) 30 chini ya orodha 30. Ambapo wamevutia wawekezaji, na pia wamepewa tuzo za Impact Google na Tuzo ya "Venture" kwa wajasiriamali. 
Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu (kushoto), akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, wakiwa na kijana mshiriki wa kongamano kutoka nchini Ghana baada ya kijana huyu kutaka ufafanuzi kwa Rais wake wa namna vijana wanavyopewa kipaumbele katika ujenzi wa uchumi wa nchi hiyo. Mkutano huo ulifanyika Lagos, Nigeria Oktoba mwaka huu.
Sehemu ya vijana walioshiriki jukwaa kubwa la wajasiriamali Afrika, lilofanyika Oktoba mwaka huu, Lagos, Nigeria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...