Manaibu Mawaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua kiwanja kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo ambapo Serikali imetoa shilingi bilioni moja kwa kila Wizara na kuelekeza kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu Wizara zote ziwe zina majengo yake ya ofisi kwenye mji wa Serikali uliopo Ihumwa mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akiambatana na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa na Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Dkt. Maria Sasabo na wataalamu wa Wizara hiyo wametembelea na kukagua eneo lenye ukubwa wa ekari 6.3 ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililopo Ihumwa mkoani Dodoma ambalo litagharimu jumla ya shilingi bilioni 1.120 na litajengwa na Vikosi vya Ujenzi, tawi la Dar es Salaam.

Kwandikwa amesema kuwa Serikali imetupa dhamana kubwa ya kuwa wakandarasi na kusimamia majengo ya Wizara zote, sisi kama Wizara tujenge vizuri kweli kweli ili tuwe mfano wa kuigwa na Wizara nyingine na tusimamie wakandarasi wengine wa JKT, NHC ambao wamepewa jukumu la kujenga ofisi za Wizara nyingine kwa kuwa sisi ndio wenye dhamana ya kusimamia wakandarasi wote nchini kama lilivyo agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa kassimu Majaliwa. Ameongeza kuwa tuko tayari kukesha na kukesha ili kuhakikisha kuwa tunafanya kazi usiku na mchana.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (wa pili kulia) wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Mawasiliano Mhandisi Dkt. Maria Sasabo (hayupo pichani) kuhusu eneo linalojengwa ofisi ya Wizara kwenye mji wa Serikali, Ihumwa, Dodoma.
Katibu Mkuu Mawasiliano, Mhandisi Dkt. Maria Sasabo (wa kwanza kulia) akifafanua  jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya kukagua eneo linalojengwa ofisi ya Wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa (wa tatu kushoto)  wakisikiliza taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Barabara Wizarani Mhandisi Hapiness Mgalula kuhusu mipango ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (wa kwanza kulia) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) wakitembea kukagua eneo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...