Wakati msimu wa Siku Kuu ukiwa unazidi kunoga, StarTimes kupitia chaneli yao ya ST Swahili wanazidi kuirudisha Bongo Movie kwenye ramani kwa kuonyesha filamu hizo kipindi hiki cha Siku kuu. 
Filamu hizi za kibongo zimeanza kuonyeshwa wiki iliyopita ikiwa ni katika jitihada za makusudi za kuiweka Bongo Movie katika chati nzuri na kutazamwa na watanzania wengi wanaopenda kufatilia maudhui ya nyumbani, pia kwa nchi za jirani.
Alhamisi hii saa 3:40 Usiku kupitia ST Swahili channel filamu ya ‘Umuhimu Wako’ inayowakutanisha Rose Ndauka, Yvonne Cherry (Monalisa) na Mama Natasha (Natashamamvi) itakuwa ikiruka kwa mara ya kwanza.Filamu hiyo inahusu binti mmoja na kijana wa kiume lakini kila mmoja wao ana safari na historia tofauti ambayo ameipitia maishani mwake. Kijana anapata misukosuko akijaribu kusimama tena baada ya mkewe kufariki na kumuachia watoto wawili. 


Upande mwingine; binti anakumbana na changamoto kwa baba yake mzazi ambaye anamuona binti huyo kama muhuni. Wawili hawa wanaingia katika mahusiano na huku wakikabiliana na changamoto zao. Baadaye wanatulia baada ya majirani zao kuwasaidia, wanaoana na kuishi maisha ya furaha.
Filamu nyingine zitakazoruka wikendi hii kupitia StarTimes Swahili ni ‘Mjerumani’ siku ya Ijumaa na ‘Milioni 10’ siku ya Jumamosi, filamu hizi za vichekesho zimesheheni mastaa wa Komedi kama vile Ringo na Mau Fundi.

Burudani hii ya kipekee inapatikana katika kifurushi cha NYOTA ambacho mteja atalipia Tsh 8000 tu kwa upande wa Antenaa ama Tsh 11,000 kwa upande wa Dish. Msimu huu wa Siku Kuu mteja atakapolipia kifurushi cha mwezi mzima atapata kifurushi cha juu zaidi na LIPA TUKUBUSTI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...