THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Vifo vya akina Mama na Watoto bado changamoto

Takwimu zinaonyesha vifo vya kina mama na watoto  bado ni Changamoto hapa nchini ambapo   kina mama 556 kati ya laki moja hufariki Dunia wakati wa kujifungua. Akizungumza Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya afya unahusu Afya ya Mama na mtoto  Mkuu wa Chuo Cha Udaktari bingwa Cha Aga Khan Prof. Hussein Kidanto amese kuwa tatizo lipo Duniani kote ambapo zaidi ya kina mama 303 kati ya laki moja wanaozaa watoto hai hufariki Dunia.

Aidha ameongeza kuwa mimba za utotoni zimeonekana kuwa Sababu kubwa ya vifo hivyo ambapo asilimia 27 ya watoto wa kike wenye umri miaka 14_16 hupata mimba za utotoni na wengine tayari wanawatoto. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ahmed Makuwani amesekuwa Serikali imefanikiwa kufanya ukarabati wa vituo vya Afya hapa nchini ili kuboresha huduma ya Afya ya mama na Mtoto.

Dkt. Makuwani ameongeza kuwa vifo vya watoto vimepungua kwa asilimia 54 katika vizazi hai elfu moja huku kwa zaidi ya miaka 10 vifo vya kina mama vikibaki kuwa palepale ambapo ni kati ya kina mama 400 hadi 600 hupoteza maisha. Naye Mkurugenzi wa wauguzi toka Hospitali ya Aga Khan Lucy Hwai amewataka madaktari na wauguzi kwenda vijijini kukidhi mahitaji ya afya kwa akina mama na watoto ambao wanachangamoto ya upatikanaji wa huduma za kiafya.
 Wadau wa Afya ya uzazi wakiwa katika mkutano wa siku mbili ilioandaliwa na na Chuo cha Udaktari Bingwa cha Aga Khan Uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Afya ya Mama na Mtoto wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Ahmad Makuwani akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Serikali ilivyochukua hatua katika utoaji wa huduma za Afya kwa Mama na Mtoto
 Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali Lucy Kwai akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Afya ya Uzazi kwa wanawake wa Tanzania katika mkutano unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Udaktari Bingwa Aga Khan Hussein Kidanto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Chuo hicho kuandaa mkutano katika kukabiliana na changamoto ya Afya Uzazi ya Mama na Mtoto Uliofanyika jijini Dar es Salaam