Na Josephine Majura na Peter Haule WFM- Mwanza
Serikali imewataka wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kuhakikisha wanatumia fursa ya uwepo wa fedha zinazotengwa na Halmashauri katika Wilaya zote nchini kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Philip Isdor Mpango, wakati wa Mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.

Dkt. Kazungu alisema kuwa, Halmashauri zote nchini hutenga asilimia tano ya mapato yake ya ndani kila mwaka ili kuwawezesha vijana na wanawake kutumia fedha hizo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwataka wahitimu wa vyuo ambao hawana ajira katika Sekta rasmi, waanzishe vikundi vya umoja wa uzalishaji mali ikiwa ni moja ya kigezo cha kuweza kupata fedha hizo.

“Serikali ya Awamu ya Tano imejidhatiti kuwaletea wananchi maendeleo endelevu kwa kuhakikisha kila mtu kwa nafasi yake anafanya kazi uzalendo, uadilifu,  bidii na maarifa lakini pia kudumisha amani na mshikamano ili kuwa na maendeleo endelevu kwa manufaa ya kizazi hiki na  kijacho.”alisema Dkt. Kazungu.
 Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Prof. Hozen Mayaya, akiishukuru Serikali kwa kuboresha Sekta ya huduma za jamii wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza ikiwa ni mahafali ya sita kufanyika katika Chuo hicho.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza, akiwataka wahitimu hao (hawapo pichani) kuchangamkia fursa zilizopo katika  mtengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupata ajira kwa kuwa wanavigezo vya ushindani wa ndani na nje ya nchi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu, akimtunuku mmoja wa wahitimu wa ngazi ya Stashahada za Uzamili wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
 Wahitimu wa ngazi ya Stashahada za Uzamili wakiwa tayari kutunukiwa vyeti wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
 Baadhi ya wahitimu wa stashahada wakipunga kofia kwa furaha baada ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza. (Picha na Josephine Majura, Wizara ya Fedha na Mipango)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...