Kutokea kusini mwa Tanzania katika mikoa ya Lindi na Mtwara, limelala bomba lenye kipenyo cha inchi 36 na urefu wa kilometa 551 kuelekea jijini Dar es Salaam. Bomba hili lina uwezo wa kupitisha gesi asilia futi za ujazo milioni 784 kwa siku na lina matoleo yapatayo 16 ambayo yamewekwa kimkakati kuruhusu uunganishwaji wa gesi kwa wateja maeneo bomba linapopita. Bomba hili linapita katika vijiji takribani 136 ambapo suala la ulinzi limefanywa kuwa ni la kushirikiana kwa kuwawezesha wananchi wa vijiji husika kutoa huduma ya ulinzi katika mkuza wa bomba. 

Kwa kuzingatia kwamba suala la elimu na uhamasishaji ni suala endelevu, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ambalo ndio msimamizi wa miundombinu hiyo limekuwa na utaratibu wa kutembelea vijiji husika na kutoa elimu juu ya umuhimu wa miundombinu hiyo kwa Taifa na namna ya kung’amua hatari na kutoa taarifa kwa mamlaka husika. 

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wanakijiji wa Somanga Simu, Afisa Uhusiano wa TPDC, Ndg. Malik Munisi alisema “TPDC inatambua mchango wa kizalendo unaotolewa na wakazi wa maeneo bomba la gesi linapopita, inatambua kwamba mlinzi wa kwanza wa miundombinu hii ni mwananchi na hivyo tutaendelea kushirikiana nanyi kila wakati kuhakikisha miundombinu hii inaendelea kuwa salama na kudumu kwa kipindi kirefu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho”. 

Nae Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka TPDC, Ndg. Oscar Mwakasege alieleza namna ambavyo TPDC hujihusisha na dhana ya uwajibikaji kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR) na kusisitiza kwamba maeneo ya kipaumbele katika kuwajibika kwa jamii ni masuala yahusuyo afya, elimu, maji na michezo. 
Wananchi wa Kijiji cha Somanga Simu wakiwa katika mkutano wa hadhara kusikiliza masuala yahusuyo usalama na ulinzi wa bomba la gesi yaliyokuwa yakizungumzwa na wataalamu kutoka TPDC .
Wananchi wa Kijiji cha Kiwanga wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka TPDC baada ya kupata elimu kuhusu masuala ya usalama na ulinzi wa miundombinu ya gesi asilia. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...