Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Kiserikali (NGOs) wametakiwa kutekeleza Kanuni Mpya za Sheria namba 24 ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Mwaka 2002 ikiwa ni lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika misingi ya uwazi na uwajibikaji.

Hayo yamebainika jijini Dodoma wakati wa mahojiano kati ya waandishi wa habari na Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Baraka Leornard wakati wa kikao baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini wanaotekeleza Sera zinazosimamiwa na Wizara.

Bw. Baraka ameongeza wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wamepitishwa katika Kanuni mpya ili kuwa na uwelewa wa kutosha katika utekelezaji wa Kanuni za utendaji wa mashirika hayo kwa ajili ya kutambua nini kinatakiwa kufanya na nini hakitakiwi kufanyika ili kuepuka kukinzana na Sheria, Kanuni na taratibu husika.

Amesisitiza kuwa mara baada ya kikao hicho Wadau watakuwa na uelewa mkubwa wa Kanuni hizo ambao utawasaidia kuweza kutekeleza wajibu wao bila kukiuka Kanuni zozote ambazo zinaenda na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Mwaka 2002. 


Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Neema Mwanga (katikati) akizungumza na wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa kikao baina ya Wizara na wadau hao wanaotekeleza Sera zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Baraka Leornard na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali BI. Tausi Mwilima. 
Wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao baina ya Wizara na wadau hao wanaotekeleza Sera zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW .


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...