Kampuni ya Selcom kwa kushirikiana na Mastercard imetoa zawadi ya Sh milioni tatu kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR katika kupokea malipo mbalimbali kwenye maeneo yao ya biashara. 

Zawadi hizo zimetolewa jana katika promosheni ya “Shinda Mtaji” iliyoanza rasmi Novemba mwaka huu kwa lengo la kuwarahisishia wafanyabiashara hao kutumia huduma ya Masterpass QR kufanya miamala mbalimbali. 

Akizungumza promosheni hiyo, Meneja Masoko wa Selcom, Juma Mgori alisema promosheni hii inamuwezesha mfanyabiashara kujishindia Sh milioni moja kila wiki kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Novemba mwaka huu hadi Januari mwaka 2019. 

Aidha, aliwataja wateja walioshinda milioni moja kila mmoja kuwa ni Boaz Wales, Hamisi Kilenga wote wa mkoani Dar es Salaam na mfanyabiashara mmoja kutoka Arusha. 

Alisema kila mfanyabiashara atakayejiunga na Masterpass QR na kuanza kupokea miamala kutoka kwa wateja, ataingia moja kwa moja kwenye droo ya promosheni kwa wiki hiyo na kupata nafasi ya kujishindia hivyo kumuwezesha kujiongezea mtaji wa biashara yake. 

“Masterpass QR ni huduma inayomuwezesha mteja kufanya malipo ya bidhaa na huduma mbalimbali kutoka kwenye akaunti ya simu au akaunti ya benki kwa kuingiza Pay Number ya mfanyabiashara au ku-skani kodi ya QR iliyopo kwenye eneo la mfanyabiashara kwa kutumia Smartphone. 
Mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Shinda mtaji’, Godfrey Kitende akionesha hundi ya Sh milioni moja aliyoshinda baada ya kukabidhiwa jana na Kampuni ya Selcom inayoshirikiana Mastercard kutoa zawadi kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR.
Mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Shinda mtaji’, Godfrey Kitende akipokea hundi ya Sh milioni moja kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Selcom, Juma Mgori. Kampuni hiyo inashirikiana Mastercard kutoa zawadi kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...