YAMETIMIA! Hatimaye warembo kutoka nchi kadhaa wanaowania taji la Miss Journalism World 2018, ambalo litafanyika hapa nchini Ijumaa ya Desemba 14, mwaka huu wamewasili.

Warembo hao waliwasili nchini jana kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), huku wachache waliobaki wakitarajiwa kuwasili leo. Wengi wa warembo hao walitamba kufanya kweli katika shindano hilo, huku waandaaji wakisema kila kitu kmekamilika. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika jijini Arusha, katika ukumbi wa Kimataifa wa Aim Mall, huku waandaaji wakisema yatakuwa ya aina yake.

Akizungumza na waandishji wa habari jana, mratibu wa shindano hilo, Samwel Chazi, alisema warembo 16 wanatarajia kuwasili kesho mchana wakipitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu. Mmoja wa warembo hao kutoka China, Chen Sitong, alisema ana uhakika mkubwa wa kushinda, kwani amejiandaa. Mratibu wa shindano hilo, Sam Chazi, aliwataja warembo hao na nchi wanazotoka zikiwa kwenye mabano kuwa ni Pauline Murati (Ufaransa), Nina Yetvushenko (Ukraine), Linda Plaude (Latvia), Fatima Kahametova (Urusi) na Zainab Mkuwu (Malawi).

Wengine ni Wioletta Tupko (Poland) na Noelia Ovejo (Hispania), Juliana Nare (Zimbabwe), Arlette Akimana (Burundi) na Chen Sitong (China). Wapo Roseline Ogunyale (Nigeria), Gisele Umwiza (Rwanda), Cassandre Joseph (Haiti), Wendy Omanga (Kenya) na mwenyeji wao Witness Kavumo (Tanzania). “Kila kitu kimekamilika, hili ni shindano la kimataifa nab ado nafasi za kudhamini zipo, hii pia ni fursa kubwa ya kuitangaza Tanzania katika sekta ya utalii,” alisema Chazi. Alitaja viingilio katika shindano hilo ni Sh 100,000 kwa viti vya hadhi ya juu (VVIP), Sh 50,000 kwa viti maalumu (VIP) na viti vya kawaida Sh 30,000

“Tumeshusha viingilio ili kuwapa fursa Watanzania wapate kushuhudia warembo hawa wa dunia pale Aim Mall kwa mara ya kwanza,” alisema Chazi.

Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Miss Journalism World wakiwa na mwenyeji wao ambaye ni mratibu wa shindano hilo, Sam Chazi (mwenye fulana) nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), walipowasili nchini jana. .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...