WATANZANIA wanaosoma nchini China wametakiwa kuwa chachu ya maendeleo, ubunifu,kujituma na kujitolea kwa manufaa ya taifa la Tanzania ikiwemo kuchangamkia fursa za maendeleo.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania nchini humo (TASAFIC) Desemba mosi mwaka huu.
Mkutano huo ulioandaliwa na Shirikisho la Watanzania wanaosoma China na Ubalozi wa Tanzania, ulilenga kuleta pamoja watanzania wanaosoma miji mbalimbali kama Dalian, Najing na Tianjing.

Alisema watanzania wanaoishi nchini humo wanapaswa kuangalia fursa za maendeleo kuwa wabunifu kujituma na kujitolea kwa manufaa ya taifa la Tanzania.“Ili Tanzania inufaike na mafanikio ya China Kiuchumi ni lazima kuwe na wataalamu wenye ujuzi na maarifa inayokwenda sambamba na teknolojia ya kisasa,”alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawakala wa elimu ya vyuo vikuu nje ya nchi, Global Education Link, Abdul Malik Mollel ameipongeza Tume ya Vyuo vikuu (TCU) kwa kuwa na utaratibu wa kuchunguza mawakala ili kudhibiti huduma hiyo.

“Tanzania tuna mawakala zaidi ya 60 , tunampa Balozi mzigo mkubwa wa kutamka leo mawakala ni matapeli…”alisema.Jumla ya wanafunzi 500 wameanza masomo katika mwaka wa masomo ya taaluma mbalimbali nje ya nchi hasa nchi za China, India, Malaysia na Ukraini chini ya wakala wa Global Education Link.Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akizungumza na wanafunzi wanaosoma china katika mkutano Mkuu wa shirikisho la jumuiya za watanzania wanosoma China ambapo aliwataka kuwa 
wabunifu,kujitolea kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji    Global Education Link,Abdulmalik Mollel akizungumza na wanafunzi wanaosoma china katika mkutano Mkuu wa shirikisho la jumuiya za watanzania wanosoma China uliofanyika katika  chuo cha  Shanyang Aerospece China
 Pichani ni Wanafunzi wakiwa katika mkutano Mkuu wa shirikisho la jumuiya za watanzania wanosoma China uliofanyika katika chuo cha Shanyang Aerospece China.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Kwa  Mkurugenzi Mtendaji Global Education Link,Abdulmalik Mollel,Mkurungezi Mwenza,Zakia Nasor.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...