Watanzania wametakiwa kuwa wamoja na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kumuombea dua katika kipindi hiki ambacho nchi inapitia kipindi cha mabadiliko makubwa ya kiuchumi huku Serikali ikikataa kupokea misaada yenye masharti ya kudhalilisha mila na desturi za Watanzania.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati akimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais Magufuli na Kuombea Amani Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa, iliyoandaliwa na Taasisi ya Kidini ya Maridhiano Tanzania, katika Ukumbi wa Mikutano wa Sabasaba,jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa maombi hayo Naibu Waziri Masauni alisema nchi sasa inapitia kipindi cha mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayosimamiwa na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli lengo ikiwa ni kuifanya Tanzania isiwe tegemezi na kupewa masharti yanayodhalilisha mila, tamaduni na dini zetu.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza
wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu
madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.Kulia ni Askofu
Silvestre Gamanywa na Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maridhiano Tanzania iliyoandaa maombi hayo, Asha Kassim.Maombi hayo
yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Sheikh
Nurdin Mangochi akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa
kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali
za Mitaa..Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar
es Salaam.
Askofu
Silvestre Gamanywa akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais
kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa
Serikali za Mitaa.Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba,
jijini Dar es Salaam.
Viongozi
wa dini wakiwa katika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka
mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa. Maombi
hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...