Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamefanikiwa kurejesha wateja 434 waliokuwa na madeni baada ya kuanzisha kampeni ya Dawasa Tunawahitaji.

Wateja hao waliokuwa wamekatiwa huduma ya maji na DAWASA wamekubali kulipa madeni yao yenye jumla ya thamani ya Milioni 204.3 kutoka maeneo mbalimbali. 

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi wa idara ya huduma kwa wateja, Ritamary Lwabulinda amesema mpaka sasa mikoa yote 10 ya DAWASA inaendelwa na kampeni hiyo inayolenga kuwavutia wateja waliokuwa wamekatiwa huduma kutokana na madeni sugu. Amesema, hadi sasa Mkoa wa Magomeni ndio unaongoza kwa kurejeaha huduma ya maji kwa wateja 81 wenye kudaiwa jumla ya Miliioni 39.44 ikifuatiwa na Mkoa wa Temeke uliofanikwa kurejesha wateja 60 waliokuwa wanadaiwa Milioni 23.01. 

Ritamary amesema mikoa mingine na kiasi cha fedha kinachodaiwa katika mabano ni Bagamoyo wateja 59 (mil 22.9), Tegeta wateja 59 (mil 27.21), Tabata wateja 49 (mil 27.52) na Kinondoni wateja 28 (mil 13.24). Sehemu zingine ni Ubungo wateja 27 (mil 17.23), Kibaha wateja 25 (mil 8.77), Ilala wateja 24 ( Mil 12.36) na Kawe wateja 22 (mil 12.58). 

Kufuatia mpango huo wa #Dawasa Tunawahitaji kwa sasa Mamlaka hukusanya kiasi cha Shilng Milion 36.41 kila mwezi baada ya wateja hao kuingia mkataba wa kulipa kidogo kidogo kila mwezi na katika kipindi kifupi cha utekelezaji wa kampeni hiyo jumla ya Milion 59.39 zimekusanywa kutoka katika vituo mbalimbali. 

Kampeni hiyo ilizinduliwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kampeni ya ' Dawasa Tunawahitaji' lengo kuu ni kuona wateja wote takribani 10000 waliokatiwa maji wanaanza kupata tena huduma hiyo. 

Kampeni hiyo itawahusisha wateja wote waliokatiwa huduma ya maji na kupitia kwa mameneja wa mikoa yote ya DAWASA kwa pamoja wakubaliane watalipa kwa miezi mingapi madeni ambayo wanadaiwa.
Mafundi wakiwa wanasoma mita ya maji ya mteja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...