Wateja wa Kampuni ya Tigo wa mikoa ya Kanda Ziwa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa. 

Akiongea katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Mecky Manyama alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali 

“Mfumo wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka MWAUWASA. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufurahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao.,” alisema Manyama 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo mkakati yetu,” alisema Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthuman Madatti 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akionyesha namna ya kutumia simu ya kiganjani kufanya malipo, wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo. Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti.

 Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG)uliofanyika jijini Mwanza leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) , wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo.Anayefuatia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo Ally Maswanya.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...