kumi
ambao wamewekewa vifaa maalum vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant)
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameanza kusikia kwa mara
ya kwanza baada ya kuwashiwa vifaa hivyo (switch on).
Watoto
hao ambao wametoka katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Dar es
Salaam, Kilimanjaro, Tanga, Pwani na Ruvuma walifanyiwa upasuaji Novemba
12 hadi Disemba 16 mwaka huu ambapo zaidi ya asilimia 90 ya upasuaji
huo ulifanywa na watalaam wa Muhimbili.Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa magonjwa ya Pua, Koo na
Masikio, Dkt. Edwin Liyombo amesema mbali na zoezi hilo la kuwawashia
vifaa vya kusaidia kusikia, lakini pia watoto wengine ambao waliwekewa
vifaa hivyo nao wamekuja kwa ajili kuangaliwa maendeleo yao na kupatiwa
elimu ya kutunza mashine hizo.
Kwa
mujibu wa Dkt. Liyombo, tangu kuanza kwa huduma hiyo katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili Juni 2017 mpaka Disemba 2018, watoto 21 tayari
wamewekewa vifaa hivyo ambapo jumla ya shilingi milioni 777 zimetumika
kwa ajili ya upasuaji huo na endapo wangepelekwa kutibiwa nje ya nchi
Serikali ingetumia shilingi Bilioni 2.1 kwa ajili ya kufanikisha
matibabu hayo.Hivyo kutokana na upasuaji huo wa ubingwa wa juu kufanyika hapa nchini Serikali imeokoa shilingi Bilioni 1.3.
“Lengo
la hospitali ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya
kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, kwani matibabu
haya yanagharama kubwa kwani kupeleka mtoto mmoja nje ya nchi kwa ajili
ya kupandikizwa kifaa cha usikivu ni shilingi milioni 100 wakati
akipatiwa matibabu hayo Muhimbili hugharimu shilingi milioni 37 kwa
mtoto mmoja,” amesema Dkt. Liyombo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuwawashia vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto 10 waliopandikizwa vifaa hivyo Novemba 12 hadi 16, 2018. Kutoka kushoto ni mtaalam wa usikivu, Fayaz Jaffer na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa Muhimbili, Dkt. Aveline Aloyce .
Wazazi wa watoto wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Dkt. Liyombo kabla ya vifaa hivyo kuwashwa tangu walipopandikizwa Novemba 12 hadi 16, 2018.
Mtoto Rehoboth Kivuyo akisikia kwa mara ya kwanza tangu wazazi wake walipobaini kwamba ana tatizo la kusikia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...