NA TIGANYA VINCENT ,RS TABORA 

WATUMISHI wa Umma wametakiwa kuacha kujiingiza katika mikopo inayowasababisha kuuza uhuru wao na kuwa watumwa kwa wakopeshaji wasio halali na ambao hawajasaliwa na Serikali. 

Kauli hiyo imetolewa wilayani Nzega na Igunga na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara wakati wa vikao vya majumuisho na Watumishi wa Wilaya hizo. 

Alisema baadhi ya wanawakopesha hawakusajiliwa na hawalipi kodi za Serikali na hivyo kuendesha biashara hiyo kinyume cha Sheria na taratibu za nchi. Waitara alisema wakopeshaji hao wamekuwa wakikopesha kwa riba kubwa ambazo zimewafanya baadhi ya watumishi kuishi maisha magumu yaliyojaa utumwa ndani yake. 

Alisema baadhi ya watumishi ambao ukopa wamekuwa wakikabidhi hata Kadi za kuchukua Fedha (ATM) kwa wakopeshaji na inapofika mwisho mwa Mwezi ndio upiga simu kwake ili waende kwenye ATM achukue fedha kwa ajili ya kulipa deni na kidogo za matumizi na baada ya hapo anarudisha kadi mdai wake. 

Waitara alisema kitendo kinafanya taarifa za mshahara wa mtumishi kutokuwa siri kwake bali kuwa wazi hata kwa mkopeshaji jambo ambalo ni kuuza uhuru wake. Aliwataka Watumishi wa umma kuishi kulinga na mishahara wanayolipwa na kujiepusha na tamaa ambazo zinaweza kuwasababisha kujiingiza katika matatizo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...