Na WAMJW - Nanyumbu, Mtwara

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ametoa onyo Kali kwa Wauguzi wote kwenye vituo vya  kutolea huduma za afya nchini wanaovunja maadili na miiko ya kazi za uuguzi ikiwemo matumizi ya lugha chafu kwa wagonjwa na wanaowapiga akina mama wajawazito wakati wakijifungua.

Ameyasema hayo  wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya Nanyumbu, akiwa katika ziara yake Mkoani Mtwara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya hasa katika msimu huu wa Biashara ya Korosho.

Waziri Ummy alisema kuwa Serikali kupitia Baraza la Uuguzi litawafutia usajili Muuguzi yeyote atakayegundulika ametenda kosa la kumpiga mama mjamzito au kumtolea lugha chafu wakati wa kujifungua.

"Tunataka kumjua huyo, ambae ni hodari sana wakupiga wanawake wajawazito, makofi wakati wakujifungua, kwa kweli huyo ni wa kumfukuza kazi, Mimi mkiniletea namfutia Leseni yake kabisa, hafanyi kazi Serikalini, hafanyi kazi Sekta Binafsi" alisema Waziri Ummy.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya wananchi wa Nanyumbu (hawapo kwenye picha), wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akipitia ubao wa matangazo ya gharama za matibabu katika Hospitali ya Rufaa Nanyumbu, akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara.
Waziri wa Afy, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisoma cheti cha mtoto aliyefikishwa na baba yake Hospitali ya Wilaya Nanyumbu ili kupata huduma za Afya.
Wananchi wa Nanyumbu wakiongozwa na Wazee waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu pindi alipokuwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...