Na Felix Mwagara, (MOHA), MARA. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. 

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nansimo, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola amesema katika Mkoa na mikoa mingineyo zoezi la kujiandikisha lilishakamilika ila wale ambao hawakuandikishwa kipindi kile ambacho Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wanaandikisha wananchi mitaani, wanapaswa kwenda katika ofisi Wilaya za Mamlaka hiyo ili waweze kujiandikisha. 

“Wapo ambao kipindi kile NIDA wanaandikisha wananchi mitaani hawakuwepo hilo nalijua, na pia kuna wale ambao kipindi kile zoezi la kuandikishwa linafanyika walikua hawajafikisha miaka 18, hao wote ambao hawajaandikishwa wanapaswa sasa kwenda kujiandikisha haraka iwezekanavyo katika ofisi za NIDA katika Wilaya zao,” alisema Lugola. 

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara aliongeza kuwa, zoezi la vitambulisho vya utaifa ni lalazima kwa kila mtanzania aliye hapa nchini, ni kosa bwa kama wewe ni raia akaamua kukaidi ikiwa Rais Dk John Magufuli ameamua kutoa vitambulisho hivyo bure bila malipo yoyote nchini. 

“Ndugu wananchi wa Mwibara na kote nchini, kupata kitambulisho ni jambo kubwa la nchi hivyo tusililinganishe na jambo lingine lolote na tusilichukulie kirahisirahisi tu, na ninawaambia baada ya mchakato huu kuisha tukamkuta mtu hana kitambulisho maelezo yake yatakuwa ni magumu kueleweka kama kweli yeye ni mtanzania halali,” alisema Lugola.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (aliyemshika mtoto), akitoka mkutanoni baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimpongeza mwanachama mpya wa CCM, Andrea Mutesigwa (kulia) ambaye amerudisha kadi ya Chadema katika Mkutano wa Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Katika mkutano wake na wananchi hao, Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...