Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameagiza halmashauri zitakazojengwa vitalu nyumba kushirikisha vijana wenye ulemavu. Waziri Mhagama ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma na Iringa kukagua maeneo yatayojengwa na kutoa mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (Green House).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo alisema kuwa katika halmashari zote 83 ambapo teknolojia ya kilimo cha kitalu nyumba itaanzishwa, idadi ya vijana 100 watakaopata mafunzo hayo ijumuishe na wenye ulemavu.

“Halmashauri zitengeneze mfumo madhubuti wa kuwashirikisha vijana wenye ulemavu katika mradi huu, kwani wanaouwezo wa kufanya kazi kama ilivyo vijana wengine na wakiwezeshwa wanaweza”, alisema Mhagama.

Pamoja na hayo, Mhagama amehimiza halmashauri hizo zisimamie vyema mradi huo kwa kuufanya unakuwa endelevu na kuwaunganisha vijana kwenye vyama vya akiba na mikopo ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kujiendeleza kiuchumi kupitia programu hiyo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa vijana na wakazi wa Mkoga alipofanya ziara ya kikazi Mkoa wa Ruvuma na Iringa kwa lengo la kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi na kutoa mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya Kilimo cha kitalu nyumba.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Bw. Ahmed Njovu akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Mkoani humo.
 Afisa Maendeleo ya Vijana Bw. Atilio Mgamwa akitoa taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama juu ya hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa programu ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.
 Mratibu wa Mradi wa Kitalu Nyumba Bi. Elizabeth Kalilowele akielezea utekelezaji wa mradi wa kitalu nyumba ulipofikia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...