Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameitaka Menejimenti ya Ofisi yake
kushughulikia kero za watumishi kwa haki na usawa ili kumaliza kero
zilizopo.
Ameyasema hayo wakati wa Mkutano
na Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu walipokutana kujadili masula
yanayowakabili wawapo kazini uliofanyika Desemba 10, 2018 katika Ukumbi
wa LAPF Dodoma.
Waziri aliwataka Watendaji wa
ofisi yake kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili watumishi kuhusu
madai mbalimbali ikiwemo; kupanda madaraja, uhamisho, usalama mahali pa
kazi na masuala ya kuzingatia afya wawapo kazini ili kuhakikisha
wanatekeeleza majukumu yao katika mazingira rafiki.
“Kama kuna motisha kubwa kwa
mtumishi ni kumsaidia kutatua kero yake inayohusiana na utumishi wake
kwa uzito unaolingana na tatizo au uhitaji wake ili kusaidia kuongeza
morali yake katika kufanya kazi.”Alisema Mhagama.Sambamba na hilo waziri aliwaasa
watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kutumia mabaraza ya Wafanyakazi katika
kujadili na kutatua kero wanazokabiliana nazo wawapo kazini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiongoza kikao cha pamoja na Watumishi wa Ofisi hiyo walipokutana akujadili masuala yao ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na kuendelea kufanya kazi kwa umoja, mkutano huo ulifanyika Desemba 10, 2018 katika Ukumbi Mikutano wa LAPF Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi yaWaziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...