Na. OWM, Kigoma.

Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Biashara, kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji unaotekelezwa katika mkoa wa Kigoma na Dodoma, umefanikiwa kuboresha Mazingira ya Biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo kwa kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 16 hadi kufikia Desemba 2018.

Mradi huo ambao utekelezaji wake unajikita katika Uwekezaji na Biashara katika Halmashauri kupitia mfuko wa (SIFF), Kuimarisha minyororo ya thamani pamoja na kuimarisha majadiliano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, tayari umefanikiwa kuboresha Mazingira ya Biashara kwa Wakulima na wavuvi wa mkoani Kigoma.

Akiongea katika ziara yake mkoani Kigoma wakati wa kukagua shughuli za utekelezaji za Baraza la Taifa la Biashara, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amefafanua kuwa Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana na Mradi huo wameweza Kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia uwekezaji kwenye miradi midogo midogo inayochochea ongezeko la ajira na kipato.

“Nimetembelea Mwalo na Soko la Samaki la Kibirizi, hapa mkoani Kigoma nimeridhishwa jinsi Mradi huu ulivyoboresha miundo mbinu ya mwalo huu katika kuhakikisha wavuvi wanapunguza upotevu wa mazao ya samaki na dagaa. Niyaombe Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya yaendelee na mfumo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha walengwa wa mradi huu wanaendelea kunufaika” Alisisitiza Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Biashara Manispaa ya Kigoma Ujiji, Festo Nashoni, juu ya Uboreshaji wa chanja za kuanika dagaa katika mwalo wa Soko la samaki la Kibirizi wakati akikagua shughuli za Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akiongea na wafanyabiashara wa Soko la Jioni la Mwanga, mkoani Kigoma, ambalo limeboreshwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza mfanyabiashara, Justina Damas, Soko la Jioni la Mwanga mkoani Kigoma, ambalo limeboreshwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...