*Ni cha ujenzi wa kiwanda cha nyuzi Chalinze

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, George Simbakalia afuatilie Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu kibali cha ujenzi wa kiwanda cha nyuzi kinachotakiwa kujengwa Chalinze. Ametoa agizo baada ya Mkuu wa mkoa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo kumuleza kuwa kuna muwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha H and J cha Chalinze ambacho ujenzi wake umekwama kutokana na mwekezaji kutopewa kibali cha ardhi.

Waziri Mkuu ametoa agzo hilo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani akiwa njiani kwenda jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwaunga mkono wawekezaji na kuwafanya wawekeze bila ya urasimu, hivyo amemuagiza kiongozi huyo wa EPZA kuhakikisha kibali kinapatikana.“Nakuagiza Mkurugenzi ufuatilie kibali hicho na nikifika Dodoma nipate majibu. Hatuwezi kuchelewesha uwekezaji nchini kwa ajili ya urasimu, kila mtendaji ahakikishe anatekeleza majukumu yake ipasavyo.”

Akizungumzia kuhusu uwekezaji katika sekta ya viwanda kikiwemo na kiwanda cha Twyford, Waziri Mkuu amesema uwekezaji huo unafaida kubwa kwani licha ya mapato ya Taifa kuongezeka kupitia kodi pia wananchi wananufaika kwa kupata ajira.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaitazama juisi aina ya Sayona Fruttis wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza juisi ya matunda cha  Sayona kilichopo eneo la Chalinze Mboga wilayani Bagamoyo, Desemba 7, 2018.    Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo na wapili kushoto ni  Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makapuni ya Motisun, Subash Patel. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama juisi aina ya Sayona Fruttis wakati alipotembelea kiwanda cha Sayona kilichopo eneo la Chalinmze Mboga wilayani Bagamoyo, Desemba 7, 2018. Wapili kushoto ni  Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makapuni ya Motisun, Subash Patel na Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo,  Omari Mgumba. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha kutengeneza juisi ya matunda  cha Sayona kilichopo Chalinze Mboga wilayani Bagamoyo, Desemba 7, 2018,  Wapili kushoto ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Motisun, Subash Patel  na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo,  Omari Mgumba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...