WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wananchi hususan wakulima wa korosho nchini baada ya kuwahakikishia kuwa korosho zao zote zitanunuliwa. Amesema Serikali kupitia Bodi ya Mazo Mchanganyiko itanunua korosho zote na hakuna korosho za wakulima nchini ambazo zitabaki bila ya kununuliwa.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra akiwa njiani kwenda Dodoma. Waziri Mkuu amesema bodi hiyo inaendelea kufanya thamini na kujiridhisha kama kweli korosho hizo zimezalishwa nchini na kuangalia viwango vya ubora.

Amesema baada ya kujiridhisha kuhusu viwango vya ubora na mkulima aliyepeleka ndiye mwenyewe ndipo taratibu za malipo hufanyika. Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kununua korosho baada ya wafanyabiashara kutaka kuzinunua kwa bei ya chini ambayo haikuwa na tija.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaresti Ndikilo akizungumza  kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  ili azungumze  wakati Waziri Mkuu alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.
Wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Terra Cashew, Leonardo Denti  (wapili kulia) wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...