Na Mwandishi Wetu-Manyoni
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii ilitoa zawadi ya Sikuu ya Krismasi yenye thamani ya shilingi 280,000 kwa wazee waishio katika Makao ya Taifa ya Wazee Sukamahela Wilayani Manyoni  kama sehemu ya kuenzi mchango wao kwa Taifa.

Akitoa zawadi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto Wizarani hapo Bw. Sebastian Kitiku aliwaambia wazee hao kuwa serikali inathamini mchango wazee katika ujenzi wa Taifa ndio maana imetoa zawadi hiyo kuwaenzi na kuwakumbuka.

Aidha Bw. Kitiku aliongeza kuwa pamoja na zawadi hiyo ya Krismasi Wizara pia inawahakikishia wazee hao kuwa itamaliza changamoto zote zinazowakabili wazee hao ili waweze kuishi katika mazingira safi na salama.

‘’Nawapa nafasi wazee kuongea na sisi ili tuweze kujua changamoto mlizonazo ili Wizara iweze kuwasikiliza na kuzifanyia kazi kwa ajili ya kuweka mazingira rafiki na salama katika makao haya.’’ Aliwaambia Wazee hao Bw. Kitiku.
 Baadhi ya Wazee pamoja na Watumishi wa Makao ya Wazee Sukamahela wakiwa tayari kupokea zawadi ya Sikuu ya Krismas kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku wa pili kulia mara baada ya kuwasili katika Makao hayo.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akikabidhi zawadi ya Siku Kuu ya Krismas kwa mwakilishi wazee waishio katika Makao ya Wazee waishio katika Makao ya Wazee Sukamahela yaliyoko nje kidogo ya mji wa Manyoni.
 Baadhi ya Wazee waishio katika  Makao ya Wazee Sukamahela wakijipatia kinywaji mara baada kupokea zawadi ya Sikuu ya Krismas kutoka kwa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea na  Wazee waishio katika Makao ya Wazee Sukamahela yaliyoko nje kidogo ya mji wa Manyoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...