Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI wa Uendeshaji wa SportPesa nchini Tanzania Tarimba Abbas amezionya timu za Tanzania hasa timu za Simba na Yanga kwa kuzitaka kuacha mzaha kwa mwaka huu katika michuano ya Kombe la SportPesa.

Tarimba amesema hayo leo Januari 15,2019 wakati anazungumzia mashindano hayo ambayo yanatarajia kuanza Januari 22 hadi Januari 27 mwaka huu na kwamba vigogo wa timu nane kutoka Tanzania na Kenya
watashiriki.Katika kuhakikisha michuano hiyo inapewa nafasi ya kuangaliwa na mashabiki wengi wa soka SportPesa imeamua kushirikiana na SuperSport kuonesha michuano hiyo.

Akizungumzia michuano hiyo Tarimba amesema kutokana na timu za Tanzania kushindwa kufanya vema, waliamua kufanya kikao na viongozi wa timu za Tanzania na waliochowaambia ni kwamba mwaka huu SportPesa hawataki mzaha kabisa.

"Safari hii tumeshirikiana na SuperSort kuonesha michuano ya SportPesa ambayo itashirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya.Hii ni mara ya tatu kufanyika kwa michuano hii na mwaka jana timu ya Golmahia walienda kucheza Uingereza.

"Kutokana na hali hiyo tulilazimika kufanya kikao kizito na viongozi wa timu za Simba na Yanga, na kikubwa ambacho tunakisema kwamba mwaka huu hatutaki mzaha.Timu hizo hatutarajii kuona wanapeleke wachezaji wa daraja la pili.Na tunaomba wasifanye kama ambavyo wamefanya kwenye michuano ya Mapinduzi kwa kupeleka wachezaji ambao hawapewi nafasi ya kutosha kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara," amesema Tarimba.

Amefafanua lengo la mashindano ya SportPesa si kupata fedha nyingi bali kukuza viwango vya soka katika nchi mbalimbali na ndio maana wamekuwa wakidhamini timu kubwa katika ligi mbalimbali duniani ikiwemo Ligi Kuu nchini Uingereza na hivyo hawataki kuona vilabu vya Tanzania vinafanya mzaha.

Tarimba amesema kwake yeye mashindano hayo ni sehemu ya kuonesha vipaji vya wachezaji na hivyo wanaimani timu ya Simba na Yanga ambayo inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kufanya vema.Amefafanua mashindano hayo yamo kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) pamoja na Shirikisho la Mpira la Mpira wa Miguu nchini Kenya.Pia amesema hata CAF inatambua na kwamba hata kusimama kwa Ligi Kuu inatokana na mashindano ya sportPesa.

Alipoulizwa kuhusu uhakika wa timu za Simba na Yanga kama kweli wataleta wachezaji hao wenye uwezo ,amejibu wameingia nao mkataba na makubaliano ,hivyo wanauhakika watashiriki vema."Kwa kutambua umuhimu wa michuano hii ndio maana tunasisitiza hatutaki mzaha,na hata uamuzi wa kushirikiana na SuperSport kuonesha michuano hii ni kutokana na kutambua umuhimu wake.Hivyo ni kuziambia timu zetu.ziache mzaha na tunaomba Yanga au Simba iwe bingwa ili acheze na timu ya Evarton ya nchini Uingereza," amefafanua Tarimba.

Ameongeza anatambua uwezo mkubwa wa timu za Simba na Yanga na viwango vya wachezaji wao, hivyo ni wakati muafaka wa kuhakikisha wanaonesha ubora wao kwenye michuano hiyo ambayo ni mikubwa ambayo ilianza mwaka 2017 katika michuano iliyofanyika nchini Tanzania ambapo mshindi Gor Mahia ilicheza na Everton hapa hapa nchini.

Asema msimu wa pili wa mashindano hayo yalifanyika huko Nakuru nchini Kenya mwaka jana na mshindi kwa mara ya pili Gor Mahia alikwenda kucheza na Everton huko Liverpool nchini Uingereza Novemba.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoise Tanzania Jacqueline Woiso amesema kwa kuwa mshirika rasmi ,SuperSport imepata idhini ya kuonesha michuano hiyo mubashara kupitia DStv.

"Tunafurahi kuujulisha umma wa Watanzania kuwa hamu yao ya kushuhudia michuano hii mubashara kupitia DStv sasa imepata jibu,watashuhudia burudani hii ya aina yake tena kuanzia kifurushi cha chini kabisa cha Bombs,amesema Woiso na kwamba michezo yote itaonekana kupitia DStv
SuperSport 9 ambayo inapatikana katika vifurushi vyote."Tumeamua kufanya hivyo ili kuwapa Watanzania fursa ya kushuhudia mashindano haya ambayo yanazidi kujipatia umaarufu kila uchao,"amefafanua Woiso.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...