NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
JUMLA ya watoto wachanga 475 wamefariki dunia baada ya akinamama 41,064 kujifungua mkoani Pwani, mwaka 2018 ,hali ambayo inaonyesha idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi kimkoa bado ipo juu. Aidha kati ya akinamama hao 41,064 waliojifungua akinamama 67 walifariki dunia kutokana na uzazi. 

Hayo yalisemwa na mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, dokta Gunini Kamba wakati mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo aliposaini hati ya makubaliano na wakuu wa wilaya ya kampeni ya kuzuia vifo vya uzazi, kampeni ambayo itafanyika kwa miezi 12 nchini. Alisema, vifo vya watoto wachanga na akinamama wanaojifungua hali hairidhishi hivyo kampeni hiyo itasaidia kupunguza idadi hiyo. 

Kamba alisema, lengo hilo linaweza kufikiwa endapo akinamama watafuata maelekezo ya kiafya wanayopatiwa wakati wa uzazi ili waweze kuvuka salama katika kipindi cha uzazi. "Vifo 67 kwa waliojifungua na watoto wachanga 475 ukilinganisha na malengo ya Kitaifa bado hali sio nzuri sana "alisisitiza Kamba. Pamoja na hayo Kamba aliwataka ,akinamama wajawazito kuhakikisha wanaanza klinik ndani ya miezi 12 ya kwanza ili kujua afya zao. 

Pia waendelee na kufuatilia afya zao kulingana na utaratibu watakaopatiwa hadi wakati wa kujifungua bila kupuuzia. "Na wakijifungua inapaswa kuhakikishwa ndani ya lisaa limoja baada ya kujifungua mtoto anyonye "alifafanua Kamba. Awali mkuu wa mkoa wa Pwani, Ndikilo aliwaasa wakuu wa wilaya kwenda kusimamia malengo hayo ili kufanikisha kampeni hiyo kiwilaya, mkoa na Taifa kijumla. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...