Salaam,

Kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Nzega Mjini na Halmashauri ya Mji wa Nzega ninapenda kutumia fursa hii kuishukuru serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutuunga mkono katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za kijamii ndani ya jimbo la Nzega Mjini.

Lakini pia ninaishukuru serikali kupitia wizara ya elimu kwa kutupatia fedha jumla ya shilingi za kitanzania Milioni Mia Tatu kumi na sita (Tzs 316,000,000) kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini ambazo kwa nyakati tofauti tuliziomba serikalini kupitia Waziri wa Elimu Mhe. Joyce Ndalichako.

Aidha, mchanganuo wa fedha hizi ni kama ifuatavyo;
1. Shule ya Sekondari Mwanzoli. 
Mwanzoli imetengewa jumla ya shilingi Milioni Hamsini (Tzs 50,000,000).
Matumizi: Fedha hii itatumika kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara.

2. Shule ya Sekondari Kitangili
Kitangili imepewa jumla ya Shilingi Milioni Mia moja na hamsini (Tzs 150,000,000)

-Matumizi:
Fedha hizi zimetolewa kwa ajili ya kukamilisha shughuli zifuatazo;
a) Ujenzi wa Utawala - 50,000,000
b) Ujenzi Madarasa 2 - 40,000,000
c) Ujenzi wa matundu 6 ya vyoo- 6,000,000
d) Bwalo na Nyumba kaya mbili - 54,000,000

3. Shule ya Sekondari Nzega
Jumla ya shilingi Milioni arobaini na sita (Tzs 46,000,000) imetengwa kwa shughuli zifuatazo;
a) Ujenzi wa madarasa mawili - 40,000,000
b) Ujenzi wa matundu sita ya vyoo - 6,000,000

4. Shule ya Sekondari Chief Ntinginya
Jumla ya shilingi Milioni Sabini (Tzs 70,000,000) ambayo matumizi yake ni kukamilisha Ujenzi wa Hosteli ya wanafunzi katika shule hii iliyopo kwenye Kata ya Nzega Magharibi.

Hata hivyo tunaendelea kuwakaribisha wadau wengine kwa ushirikiano zaidi ili kuweza kusaidia ujenzi wa mabweni kwenye kila kata ili kuongea hamasa ya ushiriki wa watoto wa kike kwenye elimu na kupambana na changamoto za umbali.

Kwa upande mwingine ninapenda kuwashukuru wananchi kwa kujitolea kwao kwenye miradi ya elimu na afya ndani ya jimbo letu bila kuwasahau Wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Mji chini ya Mkurugenzi ambao nimekuwa nikiwasumbua mara kwa mara katika kuhakikisha jambo hili linafanikiwa lakini pia katika usimamizi wa miradi inayoendelea kutekelezwa jimboni na ndani ya Halmashauri yetu.

Madiwani wa maeneo ambayo miradi hii inatekelezwa pia ninawashukuru sana kwa kuendelea kuwa na umoja na ushirikiano bila kusahau Baraza la Madiwani kwa ushauri wa mara kwa mara.

Aidha ninawashukuru watendaji wote katika Ofisi ya Mbunge kwa namna ambavyo mmeendelea kufanya kazi muda wote bila kuchoka kwa ajili ya kuhakikisha tunatekeleza ahadi na ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mwisho ninawashukuru sana Sungusungu pamoja na jumuiya zao ambao wamekuwa wakishirikiana nasi sana kwenye utekelezaji wa miradi hii na kusimamia ushiriki wa wananchi wa ngazi za chini; juhudi zenu zimesaidia sana kuamsha morali ya wananchi kuja pamoja kushiriki kwenye maendeleo.

Akhsante sana,
Hussein Bashe (Mb)
Nzega Mjini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...