NA Yeremias  Ngerangera…Namtumbo.
Mohamedi Mbawala (kasorobo)mkazi wa kijiji  cha Mgombasi wilayani Namtumbo  mkoani Ruvuma amemwokoa mtoto wake  Mashaka mbawala (17)aliyeshikwa na mamba katika mto luegu.
Mashaka Mbawala alishikwa na mamba katika mto luegu wakati wa mchana akiwa na kaka yake Juma Mbawala (21)pamoja na kijana Awadi  simba (18) wakioga  katika mto huo.
Kwa  mujibu wa Juma Mbawala ambaye  ni kaka  ya mashaka alisema walikuwa  shambani pamoja na baba yao wakilima shamba na ilipofika majira ya saa nane mchana  walimwomba baba yao ruhusa kwenda kuoga kupunguza joto na jasho mwilini kutokana  na jua kali lililokuwa linaendelea wakiwa shambani hapo.
Baba yao Mohamedi aliwaruhusu wote watatu waende wakapunguze jasho na joto mwilini na kisha warudi  shambani kuendelea na kulima  kwa kuwa shamba lao hulima mpaka kwenye ukingo wa mto huo.
Watoto hao kwa  pamoja walienda kwenye mto huo na kuanza  kutoa jasho na mara mmoja kati yao akaanza kupiga kelele za kuhitaji msaada na wenzake baada ya kumwona mamba wakaanza nao kupiga kelele na ndipo baba yao alikuja haraka  na panga na alipofika pale alimwona mwanae amechukuliwa  na mamba na ndipo alipojitupa kwenye maji na kumfuata mtoto wake na kuibua ugomvi mkali kati yake na mamba.
Mohamedi Mbawala alidai aliridhika nayeye kupoteza maisha kuliko kumwacha mtoto wake aende huku yeye akimwona alimkata panga mamba mkiani lakini mamba huyo hakumwachia mwanae  badala yake aliacha kumshika kwenye paja la mguu wa kulia akamshika kwenye  goti na alipompiga panga la pili mamba huyo aliachia kwenye goti na kushika mguu maeneo ya vidole na alipompiga panga la tatu mgongoni alikubali kumwachia mwanae huku akiendelea kupambana nae  eneo la mto huo likitapakaa damu tupu.
Baada ya mamba huyo kumwachia mwanae  alimtoa nje ya mto na kumlaza kwenye mchanga  akiwa amezimia kutokana na kunywa maji mengi alipigwa mchanga tomboni ili kuyaondoa maji  na baadae mtoto huyo aliweza kupata ufahamu na ndipo walipomkimbiza Zahanati ya Mgombasi kwa Matibabu ya awali.
Mtendaji wa kata ya Mgombasi bwana Abeid kilosa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa mtoto huyo amekimbizwa hospitali ya peramiho kutibiwa majeraha aliyopewa na mamba sehemu ya paja la mguu wa kulia ,kwenye goti na sehemu ya vidole katika mguu huo.
Afisa ardhi na maliasili bwana Saimon Sambalu alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuwahatarisha wananchi na vijiji vilivyopo kandokando na mto luegu kujihadhari  kutumia maji ya mto huo kutokana na kutapakaa mamba katika mto huo.
Aidha aliwataka wazazi katika maeneo yanayopita mto huo kutowataka watoto wao kuoga ,kuchota maji katika mto huo wakiwa peke yao kwani kwa sasa mamba katika mto huo wameongezeka hasa nyakati hizi za masika ambapo maji yanakuwa mengi katika mto huo na mamba kusambaa katika maeneo mengi wakisaka chakula alisema Sambalu.
Kijiji cha mgombasi ni miongoni  mwa vijiji vya Luegu,Mtonya na Libango wilayani Namtumbo  vilivyogubikwa na matukio ya mara kwa mara ya watu kuliwa na mamba hasa nyakati za masika .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...