Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Wananchi wanaoishi pembezoni mwa Miundombinu ya Barabara Nchini kuwa walinzi kwa kutoa Taarifa kwa vyombo husika dhidi ya wale wanaoharibu kwa makusudi miundombinu hiyo iliyojengwa kwa gharama kubwa.

Alisema wapo baadhi ya Watu waliojitoa mshipa wa fahamu kwa kuiba alama zilizowekwa Bara barani, kuchimba Mchanga au udongo pembezoni mwake jambo ambalo kama Wananchi hawatakuwa tayari kutoa ushirikiano wao kwa vyombo vya Dola  ile azma ya Serikali ya kuimarisha Sekta ya Mawasiliano inaweza kufifia.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati wa hafla ya kuizindua rasmi barabara ya Kilomita Tatu iliyojengwa kwa Kiwango cha Lami kuanzia Wawi -Mabaoni  hadi Mgogoni Chake Chake Pemba ikiwa ni mwanzoni mwa Shamra shamra za Maadhimisho ya kusherehekea Miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Alisema uzoefu unaonyesha wazi kwamba mahala popote palipojengwa Miundombinu ya Bara bara katika kipindi kifupi hutoa fursa kwa Wananchi wake kunawirika Kiuchumi kutokana na harakati za Kibiashara zinazoambatana na ujenzi wa Makaazi bora yanayolingana na uwepo wa Bara bara husika.
 Balozi Seif akizungumza na Wananchi wa Wilayua ya Chake chake katika hafla ya uzinduzi wa Barabara ya Wawi – Mabaoni – Mgogoni ndani ya shamra shamra za maadhimisho ya Sherehza kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Mheshimiwa Hamadi Ali Rashid { Gerei } akitoa shukrani kwa Serikali kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo lake kutokana na Utekelezaji sahihi wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 -2020 katika Sekta ya Mawasiliano. Picha na – OMPR – ZNZ.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiizindua Barabara ya Kilomita Tatu ya Wawi – Mabaoni – Mgogoni ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 55.
 Muonekano wa Barabara ya Wawi Mabaoni – Mgogoni iliyozinduliwa na Balozi Seif imeigharimu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zaidi ya Shilingi Bilioni 1.9.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...