Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati Serikali Kuu ikijitahidi kuondoa tofauti ya Kimaendeleo baina ya Visiwa Vikubwa na Vidogo Wananchi wanapaswa kukataa ushawishi unaofanywa na baadhi ya Watu wa kuwataka waache kutumia huduma za maendeleo zinazoimarishwa na Serikali kila kukicha.

Alisema upuuzi wa Watu hao kamwe hautaleta maana yoyote kwa vile Ilani ya Chama cha Mapinduzi inayosimamiwa na Serikali zote mbili Nchini Tanzania imeahidi kuleta mabadiliko  makubwa ya Maisha kwa kila Mwananchi bila ya kujadi utofauti wao wa Majimbo, Dini na hata itikadi za Kisiasa.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuzindua Mradi wa huduma za Umeme katika  Historia ya Kisiwa kidogo cha Uvinje kilioko Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kusherehekea kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Alisema kila Mwananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba  ana haki ya kupatiwa huduma muhimu za Kijamii, bila ya kujali anakotoka hata kama ataamua kuishi kwenye Visiwa vidogo vidogo atakuwa na haki ya kupata huduma hizo kwa faid ya ustawi wake na familia yake.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Kisiwa cha Uvinje wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Umeme Kisiwani humo. Picha na –OMPR – ZNZ.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi huduma za Umeme katika Kisiwa cha Uvinje baada ya kukamilika kwa mradi huo muhimu katika Historia ya Kisiwa hicho. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Nd. Hassan Ali Mbarouk, Kulia ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Mh. Juma Makungu na Mkuu wa Wilaya ya Wete Nd. Abeid Ali Juma.
 Balozi Seif akibonyeza kitufe kuashirika kuwaka wa Umeme katika eneo la Skuli ya Uvinje iliyomo ndani ya Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...