Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Benki za Biashara za NMB na Benki ya Posta (TPB) lengo likiwakuwasaidia wakulima wadogo wadogo kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo chini ya TADB. Makubaliano hayo yamefikiwa ili kumwezesha na kumwinua mkulima mdogo aweze kumudu kilimo chenye tija, kupunguza umaskini na kufikia malengo ya serkali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo hayo, Meneja anayesimamia Mfuko, Bw. James Mwakilima alisema Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 45 kwa mfuko kwaajili ya  kuwakopesha wakulima wadogo  sehemu mbalimbali hapa nchini.

“Katika kutimiza azma yake ya kujenga uchumi wa kati na viwanda, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 45 kwa TADB kupitia  mfuko  wake wa dhamana kwa wakulima wadogo ili wakulima waweze kujikita  kwenye kilimo chenye tija.” alisema Bw. Mwakilima

 Bw. Mwakilima alitoa wito kwa wakulima nchini kuitumia vyema fursa hiyo kwa kuwa itakuwa fahari kubwa kwa Benki ya Kilimo kuona wakulima wanainuka kiuchumi na kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa kati na viwanda kwa kuwa hakuna viwanda visivyo na malighafi.

“Ni nafasi pekee kwa  wakulima wadogo hapa nchini kuitumia vyema fursa hii kwani Benki ya kilimo ni moja ya madaraja ya kumvusha mkulima kutimiza malengo yake. alisisitiza Bw. Mwakilima.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Posta (TPB), Bw. Ramadhan Mganga alisema kuwa kupitia Mfuko huo Benki yake imefanikiwa kuwakopesha wakulima wadogo hapa nchini. Bwana Mganga alitumia nafasi hiyo  kutaja mikoa ambayo imenufaika na mikopo kuwa ni pamoja na Simiyu, Iringa na Singida.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha wakulima wananufaika na mikopo hiyo, Benki ya Posta imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa wakulima wadogo juu ya mazao gani walime na kwa wakati gani ili waweze kuwa na kilimo chenye tija

TADB imejipanga kuhakikisha kuwa inashirikiana na mabenki  ya biashara ili kunifanikisha azma ya serikali ya Awamu ya Tano ya kuleta mageuzimakubwa katika sekta ya kilimo ikiwemo kuwainua wakulima wadogo na kuchagiza maendeleo ya sekta ya viwanda. .

 Kaimu Mkurugenzi  wa Mikopo toka Benki ya Posta  Bw,  Ramadhan Mganga (wapili kulia) akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo nchni (SCGS). Mkutao ulifanyika Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Meneja Miradi wa TADB, Bw. James Mwakilima (wapili kushoto), Meneja Masoko na Uhusiano wa TADB, Bw. Said Mkabakuli (kushoto) na kulia ni Meneja Mikopo  wa Benki ya Posta Bw. Mtewele Lucius.
 Meneja Miradi wa TADB, Bw. James Mwakilima (wapili kushoto) akifafanua jambo kuhusu Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo nchini (SCGS) wakati wa mkutano na wanahabari kuhsu Mfuko huo. Kushoto kwake ni  Kaimu Mkurugenzi  wa Mikopo toka Benki ya Posta  Bw,  Ramadhan Mganga. Wengine pichani ni Meneja Masoko na Uhusiano wa TADB, Bw. Said Mkabakuli (kushoto) na  Meneja Mikopo  wa Benki ya Posta Bw. Mtewele Lucius (kulia).
Maafisa kutoka TADB na TPB wakionesha nyaraka kuhusu Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo nchini (SCGS) . SCGS inalenga kuwawezesha wakulima kukopa katika taasisi za fedha za ikiwemo benki za biashara pamoja na kuziwezesha taasisi hizo kuwa na uwezo wa kuwakopesha wakulima nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...