Na Khadija Seif, Globu ya jamii

KATIKA kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi benki ya posta nchini (TPB) imesaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara na shirika la Mawasiliano nchini (TTCL) jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya posta (TPB) Sabasaba Moshingi katika hafla hiyo amesema, utakua ushirikiano mzuri ambao utaleta mafanikio makubwa hasa kuwapa fursa wateja wa benki ya TPB pamoja na wateja wa TTCL katika kufanya mahitaji yao ya kifedha mtandaoni.

Moshingi ameeleza jinsi wateja wa benki ya TPB na wateja wa Shirika la Mawasiliano (TTCL) watakavyonufaika kutokana na maboresho ya huduma hizo  za kifedha kwa njia ya mtandao na kuwapunguzua gharama za kupanga foleni kusubiri kufanya malipo ya baadhi ya gharama au mahitaji muhimu ya kila siku .

"Ni matumaini yangu Sasa kwa wateja wetu kutoka benki ya posta(TBP) watafurahia huduma za fedha mtandao kiganjani kupitia ttcl" alisema Moshingi.


Pia mkataba huu utaweza kuleta maendeleo makubwa kwa pande zote mbili hivyo ni jinsi gani wateja watapata suluhisho la huduma za kifedha kwa haraka zaidi kupitia benki ya posta (TPB)kwa njia ya kimtandao kutokana na kukua kwa teknolojia dunia ni fursa Sasa kwa wateja wote kufanya manunuzi yao kiganjani.

Kwa upande wa Mkuu wa kitengo cha huduma za T_pesa kutoka shirika la Mawasiliano (TTCL) Moses Alphonce amesema mkataba huo utakua Na chachu pamoja na ufanisi mkubwa kutokana na kuongeza kwa wateja wengi ambao watajiunga na  mtandao wa ttcl au benki ya posta(TPB) na kunufaika na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao.

"Hata hivyo lengo la ttcl ni kuwafikia wateja wengi vijijini na mijini Alphonce kutokana na Kasi ya huduma zinazotolewa na ndio maana tumeamua kuboresha huduma za t_pesa kurahisisha ufanisi zaidi wa mahitaji ya wateja wetu "alisema Alphonce.

Pia Alphonce ameeleza kuwa muunganiko huo utasaidia wateja wote kufanya mahitaji kwa haraka zaidi na mawakala wataongeza kwa wingi kwa mwaka huu ili kufikia wateja kwa haraka zaidi.
Picha ya pamoja wakati wa hafla ya kusaini Mkataba wa makubaliano ya huduma ya fedha Mtandao kati ya  Tpb na T_pesa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...