Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA),Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ametembelea mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini na kushiriki upandaji wa miti pembezoni mwa chanzo cha Mto Ruvu.

Mwamunyange amepanda mti sambamba na wajumbe wa bodi kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji vya mto Ruvu ikiwa ndio chanzo kikubwa kinachozalisha maji kwa asilimia 88 katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.Akiwa katika ziara yake ya siku ya pili, Mwamunyange ametembelea mtambo huo ikiwa ni mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo.

Mwamunyange ametembelea mtambo huo akiwa ameongozana na wajumbe wa bodi ya DAWASA kuona namna uzalishaji maji unavyoanzia na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wahandisi wa Mamlaka hiyo.Akizungumza baada ya kumaliza kutembelea mtambo huo, Mwamunyange amesema kiwango kikubwa cha uwekezaji kimefanyika na wataalamu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata maji.

Mwamunyange amesema jitihada kubwa za serikali zinafanyika kuhakikisha wananchi wote wanapata maji hususani kwenye maeneo yaliyokuwa hayana maji kwa kipindi chote kikubwa wananchi wawe wavumilivu kwakuwa DAWASA wanafanya kazi kuwapelekea maji.Baada ya kuwasili katika mtambo huo Mwamunyange alipata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa mtambo huo na kuwataka wafanye kazi kwa juhudi kubwa ili kutimiza adhma ya serikali ya kufikia asilimia 95 ya wananchi wote ifikapo 2020.

Mwamunyange amesema, anafahamu kuna changamoto mbalimbali za wafanyakazi ila amewaahidi atazifanyia kazi atakapokutana na Sekretarieti ya DAWASA.Mbali na kutembelea mtambo wa Ruvu Chini, Mwamunyange ametembelea Tenki la maji la Changanyikeni, Busta pampu zilizofungwa Makongo kwa ajili kusukuma maji na maunganisho mapya Salasala.

Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi itaendelea kwenye maeneo mengine tofauti kwa ajili ya kujifunza na kuona namna DAWASA wanavyotoa huduma ya maji kwa wananchi wa Dar esSalaam na Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Mhandisi Arone Joseph walipotembelea mtambo wa Ruvu Chini ikiwa ni ziara ya siku tatu.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka (DAWASA) Jenerali Davis Mwamunyange akipanda miti pembezoni mwa chanzo cha Mto Ruvu wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...