Na Khadija Self,  Globu ya jamii.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr.  Hamis Kigwangwala ametengua uteuzi wa bodi ya utalii nchini  (TTB) kutokana na kutoweza kukamilisha baadhi ya maagizo aliyoyatoa katika kuboresha utalii nchini likiwemo swala la kuandaa mabango , filamu pamoja na kuanzisha studio itakayorusha na kutangaza utalii kwa masaa 24 .

Pia Waziri Kigwangala Pia ametoa kipindi cha miezi mitatu kwa watendaji wengine katika wizara yake kuwa wabunifu haswa kwa kutumia mifumo ya tekitonolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza tija pamoja kuboresha njia za matangazo ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

 Aidha ameupa siku Sa uongozi wa hifadhi ya Taifa (TANAPA) kutoa fedha ili kuweza kufanikisha baadhi ya maboresho katika utalii hasa kujenga studio hiyo na kuhakikisha bodi ya utalii nchini inatekeleza majukumu yake ipasavyo katika kuutangaza utalii duniani.

 Hata hivyo ameeleza,  bodi ya utalii itakayoundwa kuanzia sasa Ifanye tathimini katika utendaji wa kazi  kwa Kasi ili kutangaza vivutio vya utalii kuanzia nje ya jengo la bodi ya utalii na kuwepo kwa mabango,vipeperushi hasa kwenye Safari za ndege ambazo watu wa mataifa mbalimbali hutumia usafiri huo.

"Tunaweza kufanya maonyesho nchini Oman kwani tumeingia mkataba nao katika kuutangaza utalii, wao wana uchumi mzuri hivyo ni vizuri sasa kuwasukuma watalii kuja nchini kupumzika kutokana na hali ya hewa ya Oman kuwa ya joto." Amesema Kigwangwala

Ameongeza kuwa,  kwenye michuano ya watani wa jadi Simba na yanga kuna watu ambao ni vivutio vya kipekee ambavyo havipatikani sehemu nyingi hivyo Ni vizuri tukautangaza upekee huo kupitia filamu pamoja na mabango .

Aidha Kigwangala ameomba watu  Mashuhuri ambao wamepitishwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Ambao wamependekezwa kutangaza vivutio vya Utalii nchini, kupewa kipaumbele katika kupewa vifuta jasho kwani hutumia muda wao mwingi ambao wengine wangeweza kuutumia muda huo kwenye shughuli za kutafuta vipato .
Pia ameagiza  watu  hao,  kupatiwa vyeti vya utambulisho ili waweze kutambulika.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya utalii nchini(TTB)  Geofrey Meene amekiri kuwepo kwa changamoto kwa baadhi ya taasisi kama  TANAPA kuchelewesha fedha kwa ajili ya baadhi ya maboresho ikiwemo la kutengeneza studio ya kurushia matangazo.

Meene amemuomba waziri wa Kigwangala kuwapa muda na kufanya maboresho kwa Kasi inayostahiki .

Akieleza kuhusu kupatikana kwa watu mashuhuri wa kutangaza vivutio vya Utalii nchini, Meena amesema,  "Watu hawa mashuhuri tuliwapendekeza wengi lakini BASATA walipitisha majina 12 yakiwemo ya Issa Michuzi, Monalisa Mrisho mpoto pamoja na wengine Tisa. 

 Hata hivyo Meena amefafanua kuwa mchakato wa kuandaa majarida pamoja na mabango unaendelea hi vyo kufikia mwezi febuari mwaka huu utaweza kukamilika ipasavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...