Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo amemuomba Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso kuhakikisha Wilaya hiyo inapata Maji yakutosha kutokana nakuwepo changamoto kubwa ya upatikanaji wa Maji hayo.
Akizungumza na Watendaji wa Wilaya hiyo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso - Jokate ameshukuru kuwepo mradi wa Maji unaotoka Ruvu Juu, amesema mradi huo umekaa kimkakati kutokana na Wilaya hiyo kuwa na Viwanda vingi.
Hata hivyo, Jokate amesema maendeleo ya Wilaya ya Kisarawe yamekwamishwa kwa ukosefu wa Maji Safi na Salama hivyo kuna nia yakuhakikisha Maji hayo yanapatikana.
‘’Haileti maana kama Kisarawe haina Miundombinu yakuwezesha Viwanda mbalimbali kustawi, hata uwepo wa Bandari na Kiwanja cha Ndege’’, amesisitiza Jokate.
‘’Watu wengi wamekuwa na imani Kisarawe kuwa sio eneo la Makazi, wengi wanaishi Gongo la Mboto, Chanika kutokana nakukosekana huduma ya maji’’, ameeleza Jokate.
Jokate ameshukuru kuwepo ziara ya Naibu Waziri wa Maji ambapo amemuomba kuangalia kwa umakini miradi hiyo, Je inatekelezwa ipasavyo?
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso akisisitiza jambo wakati alipowasili katika Ofoisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya ziara yake yakutembelea miradi mbalimbali ya Maji Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo akizungumza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wakati wa ziara yake yakutembelea miradi mbalimbali ya Maji Wirani Kisarawe Mkoa wa Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...