Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo ameweka wazi kuwa atapambana kwa juhudi na maarifa kuhakikisha uwepo wa madini katika ardhi ya Kisarawe unaleta tija na neema kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza kuhusu hilo leo DC Jokate amesema chini ya uongozi wake kuanzia mwishoni mwa mwaka 2018 alianza mchakato wa kufanya Geological Survey/Mapping kwakushirikiana na Geological Survey of Tanzania na Ofisi ya Kamishna wa Madini Ukanda wa Mashariki.

Lengo likiwa kutambua aina ya madini na ubora wake na kiasi ambacho kitapatikana ili kuanza kuweka mikakati endelevu na yenye tija ya muda mrefu kwa wilaya na Taifa kwa ujumla.

Amefafanua madini ambayo wilaya ya Kisarawe imejaaliwa kuwanayo kuwa ni; Madini ya udongo jasi, madini aina ya chokaa, malighafi za ujenzi kama vifusi/mchanga, mawe, na kokoto.

Mwegelo amesema Kisarawe haiwezi kuendelea kuwa masikini na kuwa na upungufu wa huduma muhimu za afya na elimu wakati kuna madini katika aridhi ya kisarawe ambayo watu wa Kisarwe wamepewa zawadi na Mungu.

Ameeleza kuwa nia yake ya kushirikiana na vyombo vyote vinavyohusika kuhakikisha kunawekwa utaratibu mzuri utakao hakikisha mapato yote yanayotokana na madini wilayani Kisarawe yanawekewa utaratibu mzuri wa matumizi ikiwa ni pamoja na kuongeza na kuboresha miundombinu ya afya, elimu kama vile kujenga madarasa na kufikia lengo la kuwa na matundu ya vyoo ya kutosha ili kukidhi haja na viwango vinavyohitajika.

Pia DC Mwegelo amesema niwakati wa yeye kusimama imara na viongozi wote waliochini yake na Serikali kwa ujumla kuunganisha nguvu pamoja na kushirikisha wananchi ambao ndiyo wadau muhimu katika kuleta maendeleo.

"Naamini kuwa jambo hili litasaidia sana kutimiza muono mpana na ndoto kubwa ya Rais wa awamu ya tano na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.John Magufuli ya kulifanya Taifa la Tanzania kuwa Taifa lenye uchumi wa kati na kuwa taifa lenye kutegemewa na mataifa mengine.

" Uanzishwaji wa vituo maalumu vya biashara ya madini kama ilivyoelekezwa na kuagizwa na Rais Dk. Magufuli ni njia bora ya kuhakikisha madini yanainufaisha jamii kwa kuondoa umasikini na kuwa na jamii yenye kupata huduma bora katika nyanja zote za maisha,"amesema.

Amesisitiza ni kuwa, niwakati muafaka wa wananchi wa Kisarawe kutambua thamani ya madini yaliyopo katika kuongeza fursa za uchumi na maendeleo kwa kushirikiana na viongozi waadilifu, waanaojali uzalendo na wenye kutanguliza maslahi ya Taifa kwanza.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema niwakati sasa wa jamii yote ya Kisarawe kutambua kuwa fursa ya kuwepo madini ya aina tofauti wilayani humo ni mkombozi muhimu katika nyakati hizi ambazo Taifa la Tanzania linakua kiuchumi kwa kasi na kutumia rasilimali zake za ndani katika kukuza uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...