Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo amezungumzia ziara ambayo imefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo ambapo ameshukuru kwa kuchangia ujenzi wa madarasa manne kwa shule za sekondari Wilaya ya Namtumbo.

Ambapo Kizigo amefafanua mchango huo umekuja wakati muhimu hasa kwa kuzingatia kwamba mwaka huu wanatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wengi, hivyo kusababisha uhaba wa vyumba vya madarasa.

Akizungumzia ziara ya Katibu Mkuu huyo, leo Januari 12,2018 Kizigo amesema alianza ziara kwa kutembelea semina ya mafunzo iliyohusisha Waalimu wakuu wa shule zote za Msingi 110 zilizopo wilaya ya Namtumbo. 

"Semina hiyo ilihusu mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa takwimu unaolenga kusaidia kuwa na takwimu sahihi za shule za msingi nchini," amefafanua.

Aliwahimiza wazingatie mafunzo hayo ili iwe rahisi kwao kuutumia mfumo huo mpya.Pamoja na hayo aliwatia moyo na kuwataka wachape kazi kwani wao ndio wahandisi wanaotengeneza wataalam wa kila kada nchini.

Kizigo amewema Katibu Mku pia alitembelea Shule ya sekondari Nasuli ambapo akiwa hapo alipokea taarifa ya shule na kukagua majengo (Hostel na madarasa) yaliyojengwa kwa fedha za mradi wa EP4R. 

Pia alipata nafasi ya kusalimia wanafunzi wa kidato cha sita mchepuo wa CBG na kuwahusia wazingatie masomo na baada ya hapo wakaenda kutembelea chuo kipya cha Ufundi VETA Namtumbo ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 kwa awamu ya kwanza.

"Katibu Mkuu alionyesha kuridhishwa na ujenzi wa chuo hicho.Ammpongeza mkandarasi kwa kumaliza kujenga kwa," amesema Kizigo wakati anazungumzia ziara hiyo ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo (kushoto kwake) na viongozi wengine waandamizi wakitembelea maeneo mbambali ya chuo kipya cha VETA Namtumbo,ambapo chuo hicho kimekamilika kwa 100% kwa awamu ya kwanza. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo wakipata maelezo kutoka kwa mkandarasi wa ujenzi wa chuo hicho kipya cha VETA ndani ya Wilaya ya Namtumbo,ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo wakipata maelezo kutoka kwa mkandarasi wa ujenzi wa chuo hicho kipya cha VETA ndani ya Wilaya ya Namtumbo,ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo alipokuwa akielezea jambo kuhusu chuo kipya cha VETA Namtumbo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo alitembelea shule ya sekondari Nasuli kupokea taarifa ya shule na kukagua majengo (Hostel na madarasa) yaliyojengwa kwa fedha za mradi wa EP4R. 
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh.Sophia Kizigo akisoma taarifa ya idara ya Elimu wilaya ya Namtumbo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo,ambapo pia alitumia nafasi hiyo kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu elimu katika wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh Sophia Kizigo pichani kushoto mara baada ya kuwasili kwenye ofisi hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...