Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaagiza watendaji wa Halmshauri zote nchini kutotumia wakandarasi katika kutekeleza  miradi inayohusu Wizara  bali kutumia mtindo wa 'Force Account' yani mafundi wa kawaida katika kutekeleza miradi hiyo.

Ametoa agizo hilo mkoani Ruvuma wakati alipotembelea na  kujionea ukarabati na ujenzi katika Chuo cha Wauguzi Songea na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale katika ziara yake ya kikazi mkoani humo. Naibu Waziri huyo amefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa baadhi ya madarasa na ukuta wa Chuo cha Waganga mkoani humo ambao ungegharimu zaidi ya Shillingi 900 ambazo fedha hizo zingetumia mtindo wa 'Force Account' zingejenga zaidi madarasa hayo na ukuta.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa katika zama hizi za Serikali ya Awamu ya Tano itazingatia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za miradi ya Maendeleo na yeye kama Naibu Waziri ataisimamia kwa karibu Miradi hiyo. Amesisitiza kuwa ujenzi wote wa miradi utakaohusu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii utazingatia utaratibu wa 'Force Account' na kibali cha wakandarasi kitatolewa na Mawaziri pekee na sio vinginevyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na baadhi ya wakufunzi, wafanyakazi na wananfunzi wa  Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale mkoani Ruvuma wakati wa  ziara yake chuoni hapo kujionea Ujenzi na Ukaratabi wa miundombinu mbalimbali.
 Baadhi ya ya wakufunzi, wafanyakazi na wananfunzi wa wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo chuoni hapo kujionea Ujenzi na Ukaratabi wa miundombinu mbalimbali.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akikagua mradi wa ujenzi wa chumba cha pampu ya maji katika Chuo cha maendeleo ya Jamii Mlale unaogharinu Shillingi Millioni 3 unaosimamiwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi katika ziara yake mkoani Ruvuma kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema na Kushoto ni Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Luciana Mvula
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale mkoani Ruvuma wakati wa  ziara yake chuoni hapo kujionea Ujenzi na Ukaratabi wa miundombinu mbalimbali  kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema na Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Luciana Mvula.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...