*~ Wananchi waanika hali ilivyo*


Na Ripota wetu, Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu amefanya ziara ya kushtukiza kwenye Zahanati ya Mkoreha iliyopo Kata ya Mkoreha ili kubaini ukweli juu ya huduma zitolewazo.

Gavana Shilatu alitembelea Leo Jumatano Januari 23, 2019 ambapo amebaini uwepo wa huduma nzuri inayoghubikwa na changamoto ya uwingi wa Wagonjwa na kutoa maagizo kwa watoa huduma kuongeza kasi ya utoaji huduma.

*"Wananchi wanakiri huduma ni nzuri, nawapongeza. Japo Kuna changamoto ya uwingi wa Wagonjwa. Nawapa maelekezo Wauguzi jitahidini kuongeza kasi ya Watu kuhudumiwa kwa haraka, muhakikishe mnatoa dawa kwani nimeziona zipo nyingi.",Alisema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu amewasihi Wauguzi kuzingatia maadili, nidhamu, miiko na uwajibikaji zaidi kazini ili kuleta tija zaidi kwani maendeleo ya Watu yanategemea zaidi uwepo wa afya njema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...