Na Abdullatif Yunus - Bukoba.

Katika kutekeleza Agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Wamezindua zoezi tekeleza agizo la Mh. Rais Magufuli la kugawa Vitambulisho kwa wajasiliamali wadogo wadogo katika Halmasahauri yao, Zoezi ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Bukoba (chemba) mnamo Januari 7, 2019. 

Akizungumza mara baada ya kugawa Vitambulisho hivyo Mh. Deogratius Muganyizi Kashasha (Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba) Amewataka wajasiliamali hao kuwa mabalozi wa wengine ambao hawajapata Vitambulisho hivyo ili wafanye Hima kujipatia Vitambulisho, sambamba na kuwakumbukusha jukumu la kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg, Solomon Kimilike Amenukuliwa akisema kuwa Zoezi hilo la Ugawaji wa Vitambulisho linaendelea kwa wajasiliamali wengine ambao wameshindwa kufika katika Uzinduzi, kutokana na sababu mbalimbali na kuongeza kuwa Kuanzia Januari 09, 2019 Watakuwa na ziara ya kuzungukia Vijiji na Kata ndani ya Halmashauri ili kugawa Vitambulisho hivyo kwa Wajasiliamali wenye sifa na vigezo.

Aidha kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo amewataka wananchi hasa wafanyabiashara wakubwa kutofanya Udanganyifu kwa kuwatumia wajasiliamali wadogo kujipatia vitambulisho, na kuwa kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Tayari Vitambulisho 37 kati ya 1,317 vimegawiwa kwa Wajasiliamali baadhi ambao wamejitokeza kuchukua Vitambulisho hivyo huku wakionekana kuwa na Imani na Serikali ya awamu ya Tano, chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuwasaidia watanzania wenye hali ya chini.

Pichani ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Mh. Kashasha akimkabidhi Kitambulisho chake Mjasiliamali Kutoka Kata ya Rubale Bwn.Edisoni Nicholaus, Katikati ni Mkurugenzi Ndg. Solomon.


Pichani: Wanaonekana wajasiliamali Bi. Praxeda Rauliani, Bi. Liliani Richard na Bi Alistidia Petro wakiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa Vitambulisho vyao katika ukumbi wa Halmashauri ya Bukoba.
Makamu Mwenyekiti Mh. Kashasha akisitiza jambo mara Baada ya Kukabidhi Vitambulisho 37 kwa wajasiliamali wadogo kati ya Vitambulisho 1,317, pembeni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukoba Ndg. Solomon Kilimike.
Bwn Edisoni Nicholausi mkazi wa Rubale, akiwa ameshikilia Kitambulisho cha ke mara baada ya kukabidhiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...